Home Kimataifa Serie A katika wingu jeusi, mechi mbili zaahirishwa na Juve nao mbioni...

Serie A katika wingu jeusi, mechi mbili zaahirishwa na Juve nao mbioni kutocheza kesho

11344
0

Hivi unajua DSTV ni king’amuzi ambacho hutakiwi kukosa kuwa nacho? Utakosaje sasa wakati Cr7 naye atakuwa anaonekana live kuanzia kesho akiwa na uzi wa Juventus, nani asiyependa kuona tukio hilo?.

Okay mimi nitaangalia mtanange huo(kama utakuwepo) kupitia simu yangu kwakuwa tayari nina application yao kwenye simu yangu, lakini sasa Serie A mechi mbili zilizokuwa zipigwe Jumapili zimeahirishwa.

Mchezo kati ya Ac Milan na Genoa, na mchezo kati ya Sampdoria na Fiorentina hazitachezwa siku ya Jumapili kutokana na daraja lililoko katika mji wa Genoa kuvunjika.

Klabu mbili za Genoa na Sampdoria wote wawili wanatokea katika mji wa Genoa mji ambao ndipo ambapo daraja hili limevunjika na inatajwa watu karibia 39 wamefariki dunia.

Chama cha soka nchini Italia kimesema taarifa mpya kuhusiana na mchezo huo zitatangazwa hapo baadae lakini pia mechi zote za kesho za ufunguzi wachezaji watavaa vitambaa vyeusi kama heshima kwa waliofariki katika ajali hii.

Wakati FA wameahirisha michezo hiyo miwili, raisi wa klabu ya Juventus Andrea Agnelli amesema wanatafuta namna mchezo wao wa kesho zidi ya Chievo usifanyike.

Agnelli amesema hii ni kutoa heshima na kuifanya siku ya maombolezo kwa waliofariki, raisi wa Serie A Gaetano Micciche akisubiriwa kutoa muongozo kuhusu mechi za kesho.

Watu wengi kwa sasa wanasubiri kwa hamu kubwa kuona namna ambavyo Cristiano Ronaldo atacheza mechi yake ya kwanza ya ligi akiwa na jezi ya klabu ya Juventus.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here