Home Kimataifa Shabiki amtukana Messi baada ya kugoma kusaini jezi yake

Shabiki amtukana Messi baada ya kugoma kusaini jezi yake

7495
0

Lionel Messi hivi majuzi amesema ipo siki atarudi tena nchini kwake na kucheza soka. Messi aliwahi kuichezea klabu ya Newell kabla hajajiunga Barcelona.


Messi aliichezea Newell ya huko Argentina tokea alipokuwa na miaka 13 ingawa yeye ni mshabiki mkubwa wa klabu ya Rosario ambayo ni mahasimu wakubwa wa Newell.

“Nina imani ipo siku nitarud nyumbani kucheza soka” Messi alikiambia chombo cha ESPN.

“Nina ndoto hiyo tokea nikiwa mtoto”

“Najua ndoto haikutumia Kucheza Newell lakini siwezi kusema najutia kwa sababu nina amini muda bado upo”

Messi atakaporudi nyumbani atakutana na mojanya dabi kubwa na za kihasimu sana huko Argentine kama ilovyo Simba na Yanga hapa kwetu kama itatokea kwa Samatta kurudi hapo baadae na akaamua kuchezea Simba au Yanga.


Kuna dabi kubwa sana na ambayo huwa ngumu mno inajulikana kama dabi ya mjini Rosario. Dabi hii inahusisha timu yake ya zamani Newell’s Old Boys na timu ya mtaani kwake Rosario Central. Unaambiwa dabi hii ni moja ya mechi ya kibabe sana.

MESSI AKUMBANA NA MZOZO KATI YAKE NA SHABIKI WA ROSARIO.

Hivi majuzi kwenye uwanja wa ndege shabiki mmoja wa Rosario alimfuata Messi akimtaka asaini kwenye tisheti yake ya Rosario Central walipokuwa wametoka kucheza na Real Valladolid.

Messi ni mchezaji wa zamani wa Newell’s , na mashabiki wengi wa klabu hiyo wanajivunia sana Messi kucheza ndani ya klabu hiyo. Ni kweli Rosario ni timu ya mji wake lakini bado ana heshima kubwa na ya kipekee ndani ya Newell. Messi aligoma kusaini jezi ile na kuondoka zake. Mshabiki yule akaanza kumporomeshea Messi matusi na kusema hana pasheni na gaifa lake akimaanisha kuwa amembagua.

Juan Arango ambaye ni mwandishi aliyekuwepo eneo la tukio alidai kuwa shabiki huyo alimwita Messi “pecho frio”, kwa kiingereza ni “passionless” akimaanisha kuwa “Hajitambui au Hajielewi”

Messi wala hakupoteza muda na shabiki huyo.


Hata hivyo jarida la Marca, liliripoti kuwa mashabiki wengi wa Rosario Central walikerekwa na kitendo cha shabiki huyo mwenzao kwenda kwenye mitandao na kuanza kumtukana Messi.

Mashabiki wengi walikuwa wakishangazwa na kitendo cha mwanamke huyo kumpelekea Messi jezi ya wapinzani wake. Wanaamini kuwa tabia ile sio ya kisoka hata kidogo kwa sababu Messi anawaheshimu Newells.

“Newells na Rosario ni Mahasimu wewe unampelekea vipi Messi jezi ya mahasimu wake? Nia ya huyo shabiki ni kumchonganisha Messi na mashabiki wake na sio kupata saini yake. Lengo ya yule mwanamke hakikuwa jema” alisema shabiki mmoja wa Rosario

Mashabiki wa Rosario hawakupendezwa na tukio lile hata kidogo.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here