Home Ligi EPL Shabiki wa Chelsea asusa kuangalia mechi hadi Sarri atakapofukuzwa

Shabiki wa Chelsea asusa kuangalia mechi hadi Sarri atakapofukuzwa

4190
0

Mwandishi wa habari za michezo Tanzania, Abdul Mkeyenge ambaye pia ni shabiki wa Chelsea ametoa maoni yake kuhusu mwenendo wa The Blues kwenye ligi ya EPL.

Mkeyenge amefika mbali zaidi akitaka kocha wao mpya Maurizio Sarri afukuzwe haraka akiamini tayari amefeli.

“Kwangu Sarri namtazama kama mtu ambaye amefeli na amefeli kwenye maeneo mengi kuanzia eneo la ushambuliaji, kiungo na ulinzi.”

USHAMBULIAJI

“Timu yetu ndio imefunga idadi ndogo ya magoli, ukitazama katika timu za top 6 ni Chelsea pekeyake ndio imeshindwa kufunga mabao mengi kinachofanyika sasa hivi ni kumfanya Hazard acheze kama mshambuliaji wa kati kitu ambacho katika mpira wa kileo hakisaidii.”

“Watu pekee ambao waliwahi kufanikiwa kwa style hiyo ni Hispania lakini sikumbuki ni ya kocha gani kama ni Vecente del Bosque au mwingine ambapo tuliona Fabregas akisimama juu lakini tangu hapo aina hiyo ya mshambuliaji imeshindwa kuzilipa timu nyingi.”

KIUNGO

“Eneo ambalo limemtambulisha Kante ni kwenye idara ya kiungo wa ulinzi, yeye amemtoa Kante katikati amempeleka pembeni Jorginho ndio anacheza chini, amekuwa akipiga pasi nyingi lakini hana assist hata moja kwa upande wangu naona Jorginho anagusa mpira mara nyingi lakini hana madhara kwenye goli la mpinzani.”

SARRI AONDOKE TU!

“Ninaposikia habari zinazomhusisha Sarri kuondolewa kwangu ni taarifa nzuri kwa sababu nimezoea nikienda kwenye vibandaumiza huwa navimba nikikaa mbele nataka kila mtu ajue Mkeyenge yupo.”

“Binafsi nilikuwa nina matumaini makubwa na Sarri baada ya kumfukuza Conte nikaamini Sarri ni mtu anayekuja kutuanzishia upya Chelsea ambayo kila mtu anaitaka.”

“Chini ya Sarri timu imezidi kurudi nyuma kwa asilimia kubwa tofauti na alivyoichukua timu kutoka kwa Conte.”

“Siku hizi nimekuwa kimya hata siendi tena kuangalia mechi za Chelsea. Mara ya mwisho kuangalia mechi ya Chelsea tulifungwa na Wolves 2-1 sikuangalia tena hadi juzi tumechezea 2-0 kwa Arsenal na nikaapa sitoangalia mechi za Chelsea hadi Sarri atakapoondoka.”

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here