Home Ligi EPL Shaffih Dauda aiondoa Man United top 4, airudisha Arsenal na kuipa ubingwa...

Shaffih Dauda aiondoa Man United top 4, airudisha Arsenal na kuipa ubingwa Liverpool

20880
0

Msimu mpya wa Epl 2018/2019 unatarajiwa kuanza siku ya Ijumaa pale Manchester United watakapokipiga dhidi ya Leicester City katika dimba la Old Traford katika mchezo ambao utaoneshwa moja kwa moja katika king’muzi cha DSTV.

Sio tu mechi ya kwanza ya EPL bali msimu mzima wa ligi huu utakufikia ulipo kama kawaida kwa kupitia king’amuzi cha DSTV tena katika kiwango cha HD.

Ligi kuu inaanza baada ya dirisha la usajili ambalo limedumu kwa takribani miezi 3,pia kukawa na kombe la dunia hapo katikati na pia mechi za kujiandaa kwa ajili ya msimu mpya.

Timu zimefanya usajili ambao umebaki masaa machache kukamilika na watu wameona usajili pamoja na maandalizi, Shaffih Dauda ameona yote haya na kwa uzoefu wake ametaja timu ambazo zitashika nafasi nne za juu EPL katika msimu ujao.

Top 4 ya Shaffih Dauda 2018/2019.

1.Liverpool. Ni miaka 27 sasa tangu mwezi April mwaka 1990 Liverpool walipoifunga Qpr 2-1 na kutwaa kombe lao la mwisho la Epl na Shaffih Dauda anaamini huu ni wakato sahihi kwa Liverpool kufanya vyema.

Sababu kuu Dauda anayoona Liverpool wanaweza kutwaa ubingwa ninkutokana na namna ambavyo kocha Jurgen Klopp ameweza kumaintain ubora wa kikosi chake ambacho msimu uliopita kilicheza fainali ya Champions League na pia kuongeza nguvu mpya na sio tu nguvu mpya bali nguvu mpya hatari.

Maingizo mapya Liverpool.

Alisson Becker (As Roma) £65m.

Naby Keita (Rb Leizpg) £52.7m

Xherdan Shaqiri (Stoke City) £13m

Fabinho (Monaco) £45m

Matokeo ya Liverpool kujiandaa na msimu mpya wa Epl.

Liverpool 7 Chester Fc 0.

Borussia Dortmund 3 – Liverpool 1.

Man City 1 – Liverpool 2.

Man United 1 – Liverpool 4.

Napoli 0 – Liverpool 5.

2.Manchester City

Shaffih Dauda anaamini kwamba Man City bado wana nafasi ya kutetea ubingwa wao, timu yao hakuna aliyondoka na wamemuongeza Ryad Mahrez huku Benjamin Mendy ambaye msimu uliopita alikuwa nje sasa anarudi.

Kwa namna Pep alivyokitengeneza kikosi chake ambacho kinatengenezwa na vijana wengi bado wana nguvu ya kupambana kutetea taji lao katima msimu huu wa ligi 2018/2019.

Ingizo mapya Man City.

Ryad Mahrez (Leicester City) £60m.

Matokeo ya Man City kujiandaa na msimu mpya.

Bayern Munich 2 – Man City 3

Man City 1 – Liverpool 2

Man City 0 – Borussia Dortmund 1.

3. Tottenhan Hotspur. Tot hawajafanya usajili wowote hadi sasa japo msimu unao Eric Moura aliyetokea PSG katika dirisha la mwezi January ataonekana akiwa na jezi ya Tottenham.

Lakini kuhusi Tottenham Dauda anaona wana advantage kwa kuwa na kikosi kile kile ambacho msimu uliopita ilikuwa kati ya timu bora EPL ikimaliza katika nafasi ya tatu katika EPL.

Matokeo ya Tottenham katika kujiandaa na ligi.

As Roma 1 Tottenham 4.

Barcelona 2 Tottenham 2.

Tottenham 1 Ac Milan 0.

4. Arsenal. Baada ya miaka takribani 22 kwa mara ya kwanza msimu wa ligi 2018/2019 tutaiona Arsenal ikiwa na kocha mpya katika benchi la ufundi, ni kocha Unai Emery.

Wengi wanaamini huyu anakuja kuipa Arsenal matokeo na msimu huu watakuwa moja ya timu ngumu EPL, hata namna ambavyo wamesajili wanaonekana ni timu ambayo inahitaji matokeo.

Maingizo mapya Arsenal.

Lucas Torreira (Sampdoria) £30m.

Bernd Leno (Bayern Leverkusen) £25m.

Sokratis (Borussia Dortmund) £16m.

Stephan Lichsteiner (Juventus) bure.

Manchester United wako wapi?

Kutokuelewana kati ya kocha (Jose Mourinho) ambaye ndio mkuu wa benchi la ufundi na baadhi ya wachezaji kunaifanya United kuwa kutokuwa na hamasa kwa wachezaji na wanakosa hamu ya kucheza”

Ikumbukwe kwamba hata Jose Mourinho mwenyewe amekuwa na manung’uniko kuhusu maandalizi ya timu hiyo kwa ajili ya msimu wa ligi na huku anatajwa kutokuwa sawa na mkurugenzi wa United Ed Woodward.

Chanzo cha Mou na Woodward kutofautiana inadaiwa ni mkurugenzi huyo kutomfanikishia Mou baadhi ya usajili ambao aliutaka na ikumbukwe kwamba Mourinho amekuwa mtu wa kusajili kila wakati.

Shaffih amesema kwa kinachoendelea Manchester United kwa sasa haoni dalili ya timu hiyo kushindana na Liverpool, Man City, Arsenal na Tottenham katika msimu ujao wa EPL.

Chelsea nao vipi?

“Maurizio Sarri hana uzoefu na EPL, ni kocha mzuri na amepata matokeo mazuri na Napoli tena kwa bajeti ndogo ila EPL ni ngumu sana tofauti Serie A” amesema Dauda.

Chelsea hadi sasa wamemsajili Jorginho na mlinda lango Kepa akipishana na Courtois anayeenda Madrid huku wakifanikiwa kumbakisha Hazard hadi hivi sasa lakini Dauda haoni njia ya Chelsea kwenda top 4.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here