Home Kitaifa Shaffih Dauda atoa ya moyoni kuhusu nafasi ya uraisi wa Simba

Shaffih Dauda atoa ya moyoni kuhusu nafasi ya uraisi wa Simba

13942
0

Wakati habari ya raisi wa Simba Salim Abdallah kutogombea tena uongozi katika klabu hiyo zikiendelea kutawala, mchambuzi wa masuala ya soka Shaffih Dauda amesema haya kuhusu uamuzi wa Salim.

“Salim Abdallah aliingia kukaimu nafasi ya urais wakati viongozi wa Simba wamepata matatizo kwa hiyo wakati akikaimu ndio ikaja hiyo hoja ya mabadiliko na yeye akapitisha mchakato wa mabadiliko ambalo ndio lilikuwa jukumu lake kuhakikisha anasimamia katika kipindi cha mpito cha mchakato hadi watakapofika kwenye kipindi cha uchaguzi ambapo nafasi ya kukaimu itakwisha.

Sio hilo tu, wakati akikaimu Simba pia ilikuwa na matokeo bora uwanjani ambayo walikuwa wameyakosa kwa muda mrefu ndio maana watu wengi wakataka achukue fomu wamchague aendelee kuongoza.

Kwa mara ya kwanza naona kiongozi wa mpira ambaye alikuwepo madarakani watu wanamlilia aendelee kuwepo lakini yeye anaamua kukaa pembeni.

Hapa tunajifunza kwamba, kuna watu ambao wapo nje ya uongozi lakini wana uwezo. Hili ni fundisho kwa wanachama kwa sababu Salim hakupigiwa kura, aliingia baada ya kushinikizwa sana, hata kipindi kile wakati wa uchaguzi wa viongozi aliombwa achukue fomu agombee lakini yeye hakuamini kama anaweza kuisaidia Simba kwa kuwa kiongozi alisimamia msimamo wake wa kutogombea.

Lilipotokea hili jambo akaonesha mapenzi yake ya dhati baada ya kuonekana klabu inakwenda mrama, akakubali kuingia kuinusuru klabu na kazi ameimaliza anaamua kukaa pembeni kupisha mawazo mapya.

Amewafungua macho wanachama wa Simba ambao wanaelekea kwenye uchaguzi kwamba, kura zao ni za msingi kupita maelezo kwa hiyo wanatakiwa waangalie wagombea nani anaweza kuisaidia Simba sio nani kakupa nini ili ukapige kura.

Salim hakufanya kampeni wala hakupigiwa kura, mazingira yaliyojitokeza hapo katikati akajikuta kaingia kwenye nafasi ya juu ya uongozi ndani ya Simba na kusimamia mchakato muhimu sasa hivi wanamuona lulu.

Inawezekana kabisa kama angegombea angepingwa na asingechaguliwa kwa sababu yeye sio mtu wa ‘ujanjaujanja’, angepita mtu ambaye angewachezesha ngoma ambayo wao wanataka kucheza kwa hiyo kwenye uchaguzi ujao waangalie watu watakao wasaidia na Salim amewaachia mfano.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here