Home Ligi EPL Shaffih Dauda, Geoff Lea wapishana kuhusu Pogba wa Mourinho

Shaffih Dauda, Geoff Lea wapishana kuhusu Pogba wa Mourinho

5326
0

Ukiachana na Mourinho kupigwa chini mjadala mwingine ulioibuka kitaa ni kwamba kuna wachezaji walikuwa wanamchomesha Mourinho ili atimuliwe, Pogba anatajwa kuwa aliongoza mapambano kuhakikisha The Special One anapoteza kibarua chake.

Lakini wapo wanaomkingia kifua Pogba kwa kusema ni mchezaji mzuri lakini kocha mwenyewe ameshindwa kumtumia vizuri amsaidie kupata matokeo uwanjani mwisho wa siku akaanza kumuweka benchi.

Shaffih Dauda na Geoff Lea wamepishana kuhusu suala la Pogba na Mourinho, Geoff anamuunga mkono Mourinho na anaamini kuna baadhi ya wachezaji wamemchomesha kocha wao. Shaffih yeye anaamini Mou ameshindwa kuwatumia baadhi ya wachezaji ikiwa ni pamoja na Pogba.

GEOFF LEA

“Pogba ni miongoni mwa wachezaji ambao takwimu zinawabeba na amekuwa na kiwango kizuri msimu huu lakini takwimu hizo hizo zinaonesha kwamba hadi sasa ndio mchezaji anaeongoza kwa kupoteza mipira.”

“Kwa ushahidi wa mechi mbili za mwisho alizocheza dhidi ya Valencia na dhidi ya Southampton nafikiri kama mtu aliangalia mechi hizo hakuna mengi ya kuzungumza kuhusiana na kiwango alichoonesha Pogba.”

“Mwisho wa siku kuna tatizo ambalo wachezaji wa kizazi hiki wanalo na Roy Keane baada ya mechi ya juzi Liverpool vs Manchester United alisema: “Mimi wakati wangu nikiwa sichezi vizuri siwezi kumlaumu kocha,” hiyo ndio akili ambayo mchezaji anapaswa kuwa nayo kwa sababu mwisho wa siku unaweza kuwa na ugomvi na kocha lakini anapokupanga anakuelekeza ukashinde mechi inawezekana akakwambia tutashinda kwa kufanya hivi lakini wewe ukajiongeza kwa kuwa unaipenda timu unayoichezea na inayokulipa pengine hata kuliko kocha.

“Kwa upande wangu, wachezaji ndio wamemwangusha kocha mmoja wao ni Pogba lakini baada ya Mourinho kuondoka tutaona kama Pogba ni mchezaji mzuri atacheza vizuri.”

SHAFFIH DAUDA

“Kilichopelekea Manchester United ikamsajili Pogba ni kutokana na records zake wakati akiwa Juventus na baada ya kwenda United wafu wengi walikuwa wanalinganisha performance ya Pogba akiwa na Juve na  baada ya kwenda United halafu wakawa hawaridhiki.”

“Pogba huyohuyo akawa anapata fursa ya kucheza katika timu ya taifa ya Ufaransa bado akawa anazungumzwa tofauti na yule wa Man United.”

“Watu wanatakiwa kujiuliza, wakati Pogba anang'aa akiwa Juve alikuwa ana majukumu gani? Alikuwa anacheza kwenye nafasi gani Akiwa Ufaransa anazungukwa na akina nani? Kwa sababu akiwa Ufaransa anakuwa amezungukwa na Matuidi, Kante, yeye anakuwa mbele yao, akirudi Man United anapewa majukumu yapi?

“Akiwa Man United Mourinho anampa majukumu tofauti na anayopewa akiwa kwenye timu nyingine, kwa nini Mourinho hakumpa majukumu kama aliyokuwa anapewa akiwa na timu nyingine?

“Kama ningekuwa kocha wa Man United nisingekuwa na sababu ya kumchezesha Pogba mbali na goli, Pogba ni mchezaji mbunifu unampa watu wa style yake ambao hata sasa wapo pale Manchester. Atakuja kocha mwingine atamtumia vizuri na wachezaji walewale na timu itapata matokeo.”

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here