Home Kimataifa Shaffih Dauda yupo kwenye soka la kisasa, wanaomtukana bado wapo Analog

Shaffih Dauda yupo kwenye soka la kisasa, wanaomtukana bado wapo Analog

5436
0

Shaffih Dauda moja kati ya jina kubwa katika soka la Tanzania . Sio kwamba ameucheza mpira wa miguu kwa ngazi kubwa za kitaifa Laa.! Ila huyu Shaffih ni mchambuzi wa Soka aliepo katika ulimwengu huu wa soka kwa muda mrefu.

Ikumbukwe miaka mitano nyuma yeye kupitia Taasisi ya Clouds Media anayofanyia kazi walikuja na shindano la sports extra Ndondo cup. Shindano hili limekua likifanyika Daressalaam na viunga vyake. Limekutanisha timu ndogo ndogo za mtaani na wachezaji wale wadogo wadogo kweli katika mafanikio ya kisoka.

Hili shindano la Ndondo cup limeenda mbali sana kiasi cha kuanza na kufanyika mikoani likikutanisha sasa mikoa minne ambayo ni Mwanza, Dodoma , Mbeya , Daressalaam. Ikumbukwe hili shindano limebadili maisha ya wachezaji wengi. Wengi wao wameonekana kutoka mashindano haya na kupelekwa ligi kuu nchini (TPL). Pia mwamuzi Herry Sasii alitokea huku katika fainali ya kwanza kabisa ya Ndondo cup yeye ndo alichezesha ile mechi.

Mwaka jana alianzisha shindano la Ndondo cup lilokutanisha vijana Wadogo wenye umri wa miaka 15. Shindano ambalo lilikua na muamko mkubwa na kulikua na Ahadi kutoka kwa Wadhamini wa Ndondo cup mwakajana Ambao ni Beko kua atakae fanya vizuri katika shindano hilo atapelekwa nchini Uturuki katka klabu ya Basiktas kufanya majaribio.

Rabin Sanga ndie kijana alieonekana kufanya vizuri mwaka jana na kuteuliwa na shindano hilo kua akawakilishe taifa kwa kufanya Majaribio katika timu hiyo ya Besikstas. Tumekua tukilia kama taifa kua ni lini na sisi tutapata wakina Samatta wengi katika timu za ulaya sasa matumaini yapo kwani sio Rabin sanga tuu wapo vijana wengi ila Rabin nipende kumuongelea kwasababu ya Shaffih.

Mwaka jana mwishoni yametoka makundi ya timu za klabu bingwa Africa (Champions league) na katika makundi hayo kundi ambalo lilikua ni gumzo ni kundi la klabu ya Simba ambao wana wakilisha timu za Afrika mashariki. Katika kundi hili shaffih kwa taaruma yake na ujuzi wake katka soka alisema Simba ni under dog.

Hapa ndipo mashabiki walimponda na kumuahidii watakaposhinda wata hawata muacha. Kweli simba mechi ya kwanza dhidi ya Js soura waliweza kuondoka na Pointi tatu kwa kuwafunga Tatu. Aisee walitukana sana walikebehi sana wakizani kazi imeisha. Walipo kwenda Kongo na Misri naona kuna ukimya na nadhani wana tafakari maneno yake teh teh teh..

Shaffih yupo njiani kuelekea Uturuki na Rabin sanga kwaajiri ya kumsimamia kijana kwenye siku zake 10 za majaribio huko katika klabu ya Besiktsas. Kinacho fanyika ndo uwakilishi wa taifa na sio tulichokiona jana usiku. Mungu akubariki shaffih mipango yako itimie hawa washabiki watakuelewa taratibu walikurupuka.

RABIN SANGA katuonyeshe kua ww ndo bora mwaka jana katika Ndondo cup na hakuna mwengine ila wewe . Wale mashabiki wa simba tuendelee kuangalia zile interviews za shaffih alipo waita UNDER DOGS mtapata majibu kwanini tunasema tusiingilie taaluma za watu.

Cc.@Sativa_clan.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here