Home Kitaifa Shime aipigia hesabu Yanga “Kucheza ligi bila kuifunga Yanga si kitu kizuri”

Shime aipigia hesabu Yanga “Kucheza ligi bila kuifunga Yanga si kitu kizuri”

3092
0

Jumapili February 10, 2019 JKT Tanzania itakuwa mwenyeji kwenye uwanja wa Mkwakwani Tanga kukabiliana na Yanga kwenye mchezo wa ligi kuu Tanzania bara.

Kocha wa JKT Tanzania Bakari Shime ‘Mchawi Mweusi’ amesema kwake ni kitu kibaya kufungwa na Yanga mara mbili mfululizo kwenye ligi kwa hiyo watahakikisha hawapotezi mchezo huo kama ilivyokuwa raundi ya kwanza.

JKT TANZANIA VS YANGA

“Ni mechi nzuri kwa maana ya kwamba Yanga wametukuta tumerejea katika hali ya ushindani tofauti na wiki mbili au tatu zilizopita kwa hiyo wachezaji wangu wamesharudi kwenye mchezo na wanaweza kupambana vizuri tofauti na siku chache za nyuma.”

“Tumejipanga vizuri kuhakikisha kwamba tunapata matokeo mazuri ili kujiweka katika nafasi nzuri kwenye ligi yetu.”

MATOKEO YA MECHI ILIYOPITA

“Yanga walitufunga raundi ya kwanza magoli matatu kwenye uwanja wao wa nyumbani kwa hiyo ni haki kwetu kulipa kisasi kwa maana ya kucheza vizuri na kupata matokeo ambayo yatawafuta machungu wana-JKT Tanzania baada ya kupoteza mechi ya awali.”

“Tunawaheshimu Yanga kwamba ni timu inayopendwa na watu wengi hilo haliwezi kukwepeka lakini uwanjani tunaingia wachezaji 11 kwa 11 ambapo kwangu mimi naamini tunawachezaji bora sana kwenye timu yetu kwa sababu wachezaji wa timu hizi kubwa wanatoka kwenye timu hizi ndogo.”

SHIBOLI ON 🔥GARI LIMEWAKA

“Shiboli yupo on fire kwa sasa anafanya vizuri amekuwa anafunga mchezo hadi mchezo na hiyo imemrudishia kujiamini kwake na ninaamini kwa namna alivyo atafanya kazi nzuri kuitafutia timu yake matokeo mazuri.”

“Tumejipanga kupata pointi tatu kwa sababu hatuko vizuri sana kwenye msimamo wa ligi na ligi yetu ukiangala tofauti ya alama ni ndogo sana tunahitaji kwenda kukaa sehemu nzuri, kuwa timu bora na ili uwe timu bora lazima uifunge timu bora.”

YANGA LAZIMA WAFE

“Kucheza ligi bila kuifunga Yanga ambayo ipo mbele yako si kitu kizuri, kufungwa na Yanga mara mbili mfululizo nacho ni kitu kibaya vilevile kwa hiyo tunahakikisha hatupotezi mechi mbili mfululizo mbele ya Yanga.”

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here