Home Entertainment Simba Day imetisha nje na ndani

Simba Day imetisha nje na ndani

15582
0

August 8, 2018 Simba imeendelea na utamaduni wake wa kutambulisha wachezaji kabla ya kuanza kwa msimu mpya wa mashindano mbalimbali ikiwa ni pamoja na ligi kuu Tanzania bara.

Simba imefanikiwa kuujaza uwanja wa taifa, kwa mujibu wa takwimu za Azam TV, zaidi ya mashabiki 53,000 walikuwepo uwanjani kushuhudia sherehe ya Simba Day.

Tamasha hili linazidi kuwa kubwa kadiri miaka inavyozidi kwenda mbele, msimu huu Simba wamefanikiwa nje na ndani ya uwanja.

Ukubwa au jinsi brand yao kama taasisi inavyozidi kukua. Hakuna shaka kabisa kwa kadiri siku zinavyozidi kwenda Simba wamehakikisha wanaiweka juu timu yao.

Wamei-market brand yao ndio maana wamejaza uwanja wa taifa wakiwa wao peke yao. Ni tukio ambalo lilikuwa linaoneshwa LIVE Azam TV lakini uwanja ulijaa.

Yanazungumzwa mengi kwamba, kwakua mechi zinaoneshwa kwenye TV ndio maana viwanja havijai na vilabu vinakosa Gate Collections lakini Simba wameiua hiyo dhana, mechi inaweza ikaoneshwa kwenye TV lakini watu wakaenda uwanjani kwa ajili ya kupata msisimko ambao akiwa nyumbani hawezi kuupata.

Bado wana nafasi ya kuhakikisha wanaongeza ubunifu zaidi kwenye hii siku kwa siku zijazo ikawa tukio la kitaifa kwa sababu Simba ina mashabiki nchi nzima.

Kuna watu wanaweza kutoka mikoani kuja uwanja wa taifa lakini wapo wengi ambao hawawezi kuja. Kwa hiyo activities ambazo zitafanyika Dar wanaweza kutengeneza mfumo zikafanyika mikoani kupitia matawi yao na kuongeza mashabiki wengi zaidi kwa sababu huo ndio mtaji walionao.

Ndani ya Uwanja

Simba imeonekana ni timu ambayo itasumbua kwenye ligi ya ndani kwa sababu aina ya wachezaji waliopo wamekuwa wa daraja la juu licha ya kukutana na timu ambayo watu walikuwa wanaibeza kwamba kwa sasa imechoka.

Chama Kivutio

Mchezaji mpya wa Simba Cletus Chama amekonga nyoyo za mashabiki wengi walikuwepo uwanjani na walishuhudia kwenye TV kutokana na uwezo wake mkubwa uwanjani.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here