Home Kitaifa Simba full mipango mzee

Simba full mipango mzee

4778
0

Ni juzi tu Simba imefanikiwa kufuzu hatua ya makundi ya ligi ya vilabu bingwa Afrika, lakini tayari imeanza mikakati ya kuhakikisha inafanya vizuri katika hatua hiyo.

Rais wa Simba Suedi Nkwabi amesema kila wanapomaliza mechi, siku inayofuata inaanza mipango kwa ajili ya mechi nyingine kwa hiyo tayari wanajipanga kwa mechi zao zijazo na watatuma mwakilishi kwenye upangaji wa makundi ya ligi ya mabingwa Afrika.

“Simba kawaida yetu tukimaliza mechi siku inayofuata tunaanza mikakati ya mechi inayofuata kwa hiyo tumeshaanza mikakati yetu kwa mechi zote zinazofuata”-Nkwabi, Rais Simba SC.

“Mwakilishi wa Simba anatakiwa kwenda Misri kwa ajili ya kuhudhuria upangaji wa makundi, kanuni za Caf zinahitaji mwakilishi kuoka Simba aende, nimepata taarifa kwamba makundi yatapangwa December 28, 2018 kwa hiyo baada ya hapo mikakati itaendelea.”

“Mmwakilishi ataondoka December 27, inawezekana nikawa mimi au mtu mwingine lakini lazima Simba ipate mwakilishi atakaekwenda kwenye upangaji wa makundi.”

Faida kwa Simba kuhudhuria draw ya upangaji makundi ni kujua kanuni na taratibu za mashindano katika hatua hiyo kwa sababu hatua ya makundi ni full branded (haki zote ni mali ya Caf).

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here