Home Kimataifa Simba ichague njia sahihi kwa ajili ya msimu ujao

Simba ichague njia sahihi kwa ajili ya msimu ujao

5865
0

Na Raphael Lucas

Simba sports club ndiyo timu pekee inayotuwakilisha kimataifa hii ni baada ya Mtibwa sugar kuondolewa na Waganda KCCA, Simba imetinga hatua ya makundi baada ya kuzitoa club za Mbambane swallows ya Zimbabwe na Nkana red devils kutoka nchini Zambia

Baada ya kufuzu kwa hatua ya makundi na kupangwa kundi D

Kundi D
1. Al Ahly ( Misri)
2. As Vita (Congo)
3. Js Soura(Aljeria)
4. Simba (Tanzania)

Kwa kulitazama hili kundi ni gumu sana Simba kutoboa na kila timu inafikiria jinsi ya kupata alama 3 dhidi ya Simba. Kwa kuwalinganisha ubora na timu zingine kiuwekezaji na Kiuchezaji wao wako juu kuliko simba.


Msimamo ligi kuu Tanzania bara(TPL)

1. Yanga 50
2. Azam 40
3. Simba 33


Simba ima viporo ata akishinda vyote bado atakua nyuma ya vinara Yanga kwa pointi tano.

Kwanini simba achangue njia moja na sahihi kwake?

Moja ya lengo kubwa la Simba chini ya Muwekezaji Mohammed Dewji ni kushiriki mashindano ya kimataifa mala kwa mala na ili wafanye hivo Simba wana njia mbili tu za kuchagua ipi bora zaidi, Baada ya kutolewa kwenye hatua ya awali na Mashujaa ya Kigoma kwenye FA Simba ili washiriki Mashindano ya kimataifa kwa msimu ujao ni lazima wahakikishe eidha wanakua mabingwa wa ligi ya mabingwa Afrika kitu ambacho ni vigumu kutokea au wawe mabingwa wa ligi kuu Tanzania bara mbele ya Yanga na Azam.


Simba klabu bingwa 2003 mechi za nyumbani:

Simba 1 – 0 ASEC
Simba 0 – 0 Ismally
Simba 2 – 1 Enyimba

Simba haikufungwa mchezo wowote nyumbani.


Simba anaweza asifanikiwe katika kufanikisha hayo tajwa juu ili ashiriki mashindano ya kimataifa kwa msimu ujao Kwani Yanga na Azam wao asilimia zote wamewekeza katika kutafta ubingwa wa Tpl huku Simba akipambana na vitu viwili kwa wakati mmoja. Ni wajibu wa viongozi wa Simba na Simba yenyewe kuchagua wapi wawekeze nguvu zao ili kuhakikisha msimu ujao wanashiriki mashindano ya kimataifa Kwani pasipo hivo wanaweza jikuta wanapoteza sehemu zote mbili.


Simba vs Vilabu vya Misri
❌2018: Simba 2-2 Masry (2-2, 0-0)
❌2001: Simba 1-2 Ismailia (1-0, 2-0)
☑️2003: Simba 2-2 Zamalek (1-0, 1-0)
❌1996: Simba 3-3 Mokaoulun(3-1,0-2)
❌1978: Simba 2-3 Al Ahly (2-1, 2- 0)
❌1985: Simba 2-3 Al Ahly (2-1, 2-0)


Kwa hesabu za kawaida Simba ni vigumu sana kuchukua Champions league ya Africa kwahiyo kama wanalitambua hilo ili washiriki kwa msimu ujao ni lazima warudi nyuma na kupambana kwenye ligi ya ndani kuliko kuwekeza nguvu sehemu ambayo ni ngumu zaidi kwa upande wao.

“Viporo vyenu vileni huku mkiwaombea Yanga na Azam wasahau kua Kuna Simba nyuma yao”

By Raphael Lucas(udom)
0710690782/0764764449


TAARIFA

Bei ya tiketi ni Tsh. 100,000.

Huduma watakazopewa siku ya mchezo;
– Watakaa sehemu ya VIP A.
– Wataacha gari zao hoteli ya Serena na kuchukuliwa na basi maalum kwenda na kurudi Uwanja wa Taifa wakisindikizwa na Polisi.
– Wapatewa jezi mpya za Simba.
– Watapata viburudisho.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here