Home Kitaifa Simba kwenye mtego wa Singida

Simba kwenye mtego wa Singida

4782
0

Simba itakuwa mwenyeji wa Singida United kwenye mchezo wa ligi kuu Tanzania bara unaochezwa leo December 29, 2018 uwanja wa taifa.

Ni mechi muhimu kwa timu zote lakini presha kubwa ipo kwa Simba kwa sababu ndio wanaowania ubingwa wa ligi, michuano ya FA Cup wameshapigwa chini kwa hiyo njia pekee ya kurudi michuano ya kimataifa ni kushinda taji la ligi la sivyo wawe mabingwa wa Afrika jambo ambalo ni gumu kwao lakini kwenye mpira inawezekana.

Kwa sasa Singida hawapo vizuri kama ilivyokuwa msimu uliopita baada ya kuondokewa na kocha pamoja na wachezaji wengi kwa hiyo upinzani wao kwa Simba unaweza usiwe unaotarajiwa japo wanaweza kuja na ‘surprise’.
.
Msimu uliopita Simba ilishinda mechi zote za ligi dhidi ya Singida United nyumbani na ugenini. Wakati Singida ikiaminiwa kutoa changamoto kwa Simba ilichezea kichapo cha 4-0 uwanja wa taifa kabla ya kupigwa 1-0 uwanja wa Namfua mechi ambayo Simba walikuwa wakisherekea ubingwa baada ya Yanga kupoteza dhidi ya Mtibwa Sugar.

Simba ipo nafasi ya 3 kwenye msimamo wa ligi ikiwa na pointi 30 baada ya kucheza mechi 13, Singida United yenyewe ipo nafasi ya 12 kwa pointi zake 19.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here