Home Ligi EPL Simba vs Mtibwa, Chelsea vs Arsenal, Chievo vs Juventus, Jumamosi flani ivi...

Simba vs Mtibwa, Chelsea vs Arsenal, Chievo vs Juventus, Jumamosi flani ivi …….

9672
0

Watoto wa mjini wanasema Jumamosi flani ivi amazing, baaasi hii leo ndio Amazing haswa kwa sisi watu wa soka na remote hazichezi mbali na mikono yetu.

Simba vs Mtibwa. Mnyamaa ambaye msimu huu hakuna asiyeogopa kucheza naye atakuwa pale Kirumba kwenye mchezo wa ngao ya jamii kati yake na wakata miwa wa Mtibwa Sugar.

Maingizo mapya kama Meddy Kagere, Paschal Wawa, Hassan Dilunga, Adam Salamba ndio muda wao haswa kuonesha kile ambacho kiliwapeleka Simba katika msimu huu.

Ni mchezo ambao unavutia lakini sio mchezo mrahisi kama ambavyo mashabiki wengi wa Simba wanauangalia, uzoefu wa Mtibwa katika mechi kubwa kama hizi na upya wa wachezaji wa Simba unaweza kuifanya mechi hii kuwa ngumu.

Chelsea vs Arsenal. London Derby hii, kati ya vitu ambavyo vinaifanya EPL ni msisimko wa Derby kama hizi, mara zote Derby kati ya Chelsea na Arsenal imekuwa ngumu haijalishi iko katika mazingira gani.

Wakati Maurizio Sarri akitafuta ushindi wa pili mfululizo tangu ajiunge na EPL, Unai Emery yeye atakuwa na jaribio la kukwepa kipigo cha pili mfululizo tangu ajiunge na ligi kuu Uingereza.

Pierre Aubameyang, Mesut Ozil watakuwa akijaribu kutafuta ushindi wao wa kwanza EPL huku Joginho akitafuta rekodi ya kuwa mchezaji wa nne Chelsea kufunga mechi zake 2 mfululizo za mwanzo Chelsea.

Chievo vs Juventus 19:00. Dunia itaelekeza macho yake pale Stadio MarcAntonio Bentegodi kumungalia Cristiano Ronaldo ambaye hii leo kwa mara ya kwanza atakuwa akicheza mchezo wake wa kwanza Serie A.

Baada ya kuitumikia Real Madrid kwa takribani miaka 9 kwa mafanikio makubwa, safari ya Cr7 kutafuta mafanikio nchini Italia inaanza hii leo katika mchezo wao dhidi ya Chievo.

Unaangalizia wapi mitanange hii?!!

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here