Home Uncategorized Simba walizidiwa wapi?

Simba walizidiwa wapi?

4880
0

Napenda kuwapa Hongera As Vita ya nchini Congo, kwa kutumia uwanja wake wa nyumbani kupata ushindi dhidi ya muwakilishi wetu peke kutoka nchini Tanzania Simba, mchezo huo uliyomalizika kwa mabao 5-0 hakuna Mtanzania, alitegemea kipigo hicho cha mabao mengi katika mchezo huu.

Simba ilifeli kwenye mchezo huu katika idara tofauti idara ya Kwanza katika safu ya ulinzi imefeli vipi sehemu hiyo.

Simba kwenye mchezo huu mabeki wa kati wa klabu hiyo Wawa na Juuko, muda mwingi walikuwa wakifanya makosa katika idara hiyo pengine me nahisi ilikuwa presha ya mchezo muda mwingi timu ilikuwa inacheza nyuma zaidi walishindwa kuugawa uwanja kwa maana ya kuwakimbia juu washambuliaji wa As Vita.

muda mwingi washambuliaji wa As Vita wakiongozwa na Makasu, na Ngoma, walitumia upenyo huo kuwazibu makosa kama haya pia katika mchezo wa awali dhidi ya JS Saoura, walikuwa wakiyafanya ulikuwa sio umakini wa washambuliaji hao.

Wawa, ni mzuri beki mwenye uwezo mkubwa wa kupandisha timu na kushambulia muda mwingi alikuwa akicheza nyuma kwa sababu huenda alijua udhaifu wake kama hana spidi na kuwamua kucheza kwa tahdhari unakuta na timu yenye washambuliaji bora kwa nini usifungwe? pale unapofanya makosa mwenzako anayatumia.

Ukimuangalia Juuko alikuwa na presha muda mwingi alishindwa kuelewana na Wawa, hii ni presha na amekuwa hana uzoefu pengo la Erasto Nyoni, linaonekana sijamaanisha kama angekuwa Nyoni, wasifungwa bali uwahi ungeonekana Wawa, akiwa na Nyoni, tunaona mabadiliko makubwa.

Simba, wameadhibiwa na makosa katika idara ya mipira miwili ya Kona mabeki wa kati wa Congo, Makwekwe, na Bopunga, wanaruka wakiwa free hii inaonyesha uzembe wa hali ya juu.

Katika idara ya Kiungo mwalimu alianza na plan nzuri katika idara hiyo kuwanzisha viungo wakabaji watatu Mkude, Kotei na Mzamiru, kipindi cha Kwanza mbinu zilifeli Mzamiru alichezwa Kiungo mkabaji wa pembeni kwa maana Congo, ni wazuri kwenye kufanya mashambulizi wakitokea pembeni Mzamiru alishindwa kuendana na kasi ya mchezo me nilitegemea kipindi cha pili angekuja na mbinu zifuatazo.

Angemtoa Mzamiru angeingia Kichuya Kiungo mshambuliaji wa pembeni kusaidia sukuma mashambulizi akitokea pembeni ni mzuri kwenye kutengeneza nafasi na kulazimisha beki afanye makosa.

Angemtoa pia Kotei angebaki na Kiungo moja mkabaji ambaye ni Mkude ili timu icheze angemuingiza Dilunga, ni mzuri kwenye kushambulia kutengeneza nafasi timu katika idara ya Kiungo kulikuwa hakuna Kiungo wa kukaa na mpira.

Katika safu ya ushambuliaji Okwi, Kagere leo wameshindwa kufanya kile kitu ambacho watu walikuwa wanakitegemea kwa sababu mpira mbele ilikuwa haiji na ikawa inafanya muda wowote waje chini na kuwapa uhuru walinzi wa As Vita.

As Vita katika idara ya ulinzi walikuwa wamekamilika walicheza vizuri sana idara ya Kiungo walikuwa ni wazuri walikuwa wana spidi na wanaamuzi ya haraka idara ya ushambuliaji pia walistahili ushindi hii ndo faida ya kutumia uwanja wa nyumbani.

Azizi_Mtambo15

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here