Home Ligi Kuu Bara Simba ya Kagere haitamwacha mtu salama

Simba ya Kagere haitamwacha mtu salama

11478
0

Medie Kagere ni moja ya majina mashuhuri katika ligi za Uganda, Kenya na Rwanda.

Mshambuliaji Kagere ni moja kati ya wachezaji tishio sana hapa Afrika Mashariki. Msimu wa mwaka 2016 waandishi wa habari walimpa tuzo ya mchezani wa thamani zaidi ligi kuu Kenya.

Mchezaji huyu wa zamani wa Gor Mahia hivi majuzi alipata uraia wa Rwanda ambayo itampa uhuru wa kuichezea Amavubi tena tokea mwaka 2011.

Mchezaji huyo mwemye miaka 32 sasa alizaliwa kule Uganda lakini ni Mnyaruanda. Amevichezea vilabu vya Rwanda kama vile Rayon Sports, SC Kiyovu Police FC na Atraco FC. Amechezea vilabu vya Uganda kama vile Mbale Heroes na Masaka LC, na klabu ya Tunisia ya Esperance Sportive de Zarzis.

Wachezaji wengine waliopewa uraia wa Rwanda ni Hussein Cyiza (Mukura), Jimmy Mashingirwa ‘Mbaraga’ Kibengo (AS Kigali), Andre Fils Lomami (Kiyovu) na Peter ‘Kagabo’ Otema (Musanze).

Wachezaji zaidi ya 60 walifutiwa uraia wao baada ya kugudndulika kuwa walifoji vyei vyao vya uraia. Hilo lilitokea baada ya Rwanda kuondolewa kwenye michuano ya kufuzu AFCON 2015 Baada ya kugundulika kuwa kuna mchezzaji akitumia vyeti viwili kwa majina tofauyi ajulikanae kama Dady Birori, raia wa Congo ambaye paspoti yake pia alijukikana kama Agiti Tady Etakiama.

Tuachane na hayo

Meddie Kagere miaka minne iliyopita alisajiliwa rasmi Gor Mahia. Wakati ule alikuwa mfungaji bora wa CECAFA akiwa na Mabao matano.

Mwaka jana mwezi wa 10 bao la Meddie Kagere liliipatia Gor Mahia ubingwa wa 16 wa ligi kuu nchini Kenya baada ya kuwafunga Ulinzi Stars 1-0 kwenye uwanja wa Kericho Green Stadium. Hilo lilikuwa bao lake la 11 kwenye ubingwa SportPesa Premier League.

Muunganiko wa Tuyisenge na Kagere ulizalisha mabao 23

Msimu wake wa mwisho uliisha na klabu yake haikuwa tayati kumuongezea tena mkataba. Kagere aliipatia klabu hiyo makombe mawili ya ligi.

Akatua Simba. Mechi yake ya kwanza dhidi ya Rayon Sport ya kule kwao akaweka kamba moja.

Anaonekana kuwa ni mchezaji tishio. Mchezo wa leo wa ufunguzi wa ligi ameweka tena kamba dhidi ya Tanzania Prisons. Ni suala la kijiuliza je muumganiko wa Okwi, Bocco na Kagere utamuacha nani salama. Kagere amewahi kucheza vilabu vya Ulaya Okwi nae pia amecheza klabu ya Ulaya ya nchini Denmark ya SønderjyskE. Kagere amecheza Tunisia sawia na Okwi.

Nani atazima moto wa hawa jamaa?

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here