Home Kitaifa Simba yashusha mrithi wa Okwi

Simba yashusha mrithi wa Okwi

16543
0

Mshambuliaji na nahodha wa Nkana FC ‘Red Devils’ Walter Bwalya anakaribia kujiunga na Simba kuziba nafasi itakayoachwa na Emanuel Okwi ambaye atajiunga na Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini.

Bwalya atajiunga na Simba kwa mujibu wa kanuni na taratibu za Caf ambapo timu zilizofuzu hatua ya makundi ya mashindano ya Afrika hupewa fursa ya kuongeza wachezaji ili kuimarisha kikosi.

Kama unakumbuka, juzi Bwalya aliifungia Nkana goli pekee wakati ikipoteza mchezo wake wa marudiano wa ligi ya mabingwa dhidi ya Simba uwanja wa Taifa.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here