Home Kimataifa Simbu apenya Olympic 2020

Simbu apenya Olympic 2020

2314
0

Wanariadha wa Tanzania Alphonce Simbu na Augustino Sulle wamefanikiwa kufuzu kwa michezo ya Olympic itakayofanyika jijini Tokyo, Japan mwakani.
.
.
Wanariadha hao wamefanikiwa kufuzu baada ya kukimbia kwa muda mzuri kwenye mbio za Lake Biwa Marathon zilizofanyika Osaka Japan ambazo zinatambulika na kupitishwa na shirikisho la riadha la dunia.
.
.
Katika mbio hizo ambazo zilikuwa na ushindani kutoka wanariadha mbalimbali duniani, Simbu ambaue ni mshindi wa medali ya shaba ya dunia alimaliza katika nafasi ya 6 akiandika rekodi yake mpya ya akitumia saa 02:08:27. Rekodi ya awali ya Simbu kabla ya mashindano hayo ilikuwa saa 02:09:10 aliyoiweka London Marathon.
.
.
Kwa upande wa Sulle ambaye anashikilia rekodi ya taifa Marathoni ya saa 2:07:04 aliyoiweka Toronto, Canada mwaka jana, amemaliza nafasi ya 17 akitumia saa 02:12:42.
.
.
Muda wa kufuzu Olympic ambao unaanza kutambuliwa kuanzia January mwaka huu ni saa 02:14 kwa wanaume.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here