Home Ligi Kuu Bara Singida United na Alliance ya Mwanza wamepata tabu leo

Singida United na Alliance ya Mwanza wamepata tabu leo

9629
0

Singida leo wamepoteza mchezo wake wa kwanza wa ligi wamepata kipigo kutoka kwa klabu mpya ya Biashara United. Singida united huu ni mchezo wao wa pili ufunguzi na zote wanapoteza

Msimu wa 2017/2018

Mwadui 2-1 Singida

Msimu 2018/2019

Singida 0-1 Biashara

Huu ni mchezo wao wa 13 tokea waanze kutumia uwanja wa Namfua kwenye michezo ya ligi kuu. Msimu uliopita katika michezo yake 12 ndani ya uwanja wa Namfua walipoteza michezo mitatu pekee.

Mpaka kufikia sasa Singida ndani ya Namfua imeshinda mabao 14 pekee na kufungwa mabao 12.

Klabu mpya ya Alliance ya jijini Mwanza imeshindwa kufurukuta mbele ya wababe wa mji huo pia Mbao Fc ya Mwanza kwa kuruhusu kufungwa bao 1 kwa 0.

Huu ulikiwa mchezo wa 3 wa Ufunguzi kwa Mbao Fc.

Mchezo wa kwanza ilikuwa msimu wa 2016/17
Stand United 0-0 Mbao

Mchezo wa Pili ilikuwa msimu wa 2017/18
Kagera Sugar 0-1 Mbao

Mchezo wa tatu ni huu wa leo
Alliance 0-1 Mbao Fc

Nimebahatika kuongea na msemaji wa klabu ya Alliance Bwana Lucas Mwafulange

Nilimuuliza vipi wameuonaje mchezo wao wa leo
“Kwa sasa tutakaa kimya hatutaki kupiga makelele isije ikatokea siku tukazidiwa tukapiga mayowe mkashindwa kutusaidia”

Tumefungwa ni sehemu ya Mchezo. Tumefungwa bao la mapema labda Mungu hajapanga iwe upande wetu. Mimi nina amini kila sauti ya radi ina sababu zake. Uwanjani leo mashabiki walijaa sana utadhani ni Simba na Yanga. Haijawahi kutokea Mechi za Mbao wakajaa hivi.

Kila mtu ameondoka kwa masikitiko kwa sababu timu bora na iliyocheza vizuri imefungwa

Kikosi chetu ni imara. Hatuhitaji majina makubwa. Unaweza kuwa na mwili mkubwa na ukawa bogasi tu.

Mchezo ujao tutacheza na African Lyon mchezaji pekee atakaye ukosa mchezo huo ambaye ni Juhudi Filemon aliyechanika nyama za paja”

Michezo mingine LigiKuuTanzaniaBara

FT’ Ruvu Shooting 0-1 Ndanda

FT’ Alliance 0-1 Mbao

FT’ Coastal Union 1-1 Lipuli FC

FT’ Singida United 0-2 Biashara

FT’ Kagera Sugar 2-1 Mwadui FC

FT’ Simba SC 1-0 Tanzania Prisons

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here