Home Kitaifa Singida waipigia hesabu Mwadui

Singida waipigia hesabu Mwadui

7699
0

Na Tima Sikilo

KOCHA wa Singida Unite Hemed Morocco, amesema kikosi chao kitawavaa Mwadui huku wakiwakosa wachezaji wao wawili Jamal Mwambeleko na Kennedy Juma walio pata majeruhi katika mchezo uliopita wa Ligi Kuu.

Singida kesho wanatarajia kuvaana na Mwadui FC  katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara kwenye Uwanja wa Namfua uliopo mkoani humo.

Morocco amesema kikosi chake kimejiandaa vizuri japo kuna baadhi ya wacheza hawatakuwepo kwakuwa bado hawajajiunga na timu pamoja nahao wawili walioumia katika mchezo wa kwanza.

Morocco amesema, mchezo wao wa kwanza wamepoteza wakiwa katika uwanja wao wa nyumbani hivyo hawapo tayari kupoteza tena katika uwanja wao japo lolote linaweza kutokea.

“Kikosi kipo vizuri japo hakijakamilika maana kuna baadhi ya wachezaji bado  hawajajiunga na timu na tutawakosa Mwambeleko na Kennedy ambao waliumia katika mchezo uliopita,” amesema Morocco.

Mchezo wao wa kwanza wa ligi Singida walichezea bao 1-0  kutoka kwa Biashara United ya mkoani Mara.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here