Home Ligi EPL Sio Van Djik pekee yake, tusiwe wachoyo

Sio Van Djik pekee yake, tusiwe wachoyo

5843
0

Nimeona mara kadhaa walio wengi wanamsifu sana Van Djik kuwa amekuwa mchezaji wa muhimu zaidi kwenye kikosi cha Liverpool. Bila shaka. Hakuna ubishi kuwa kiwango cha Van Djik ni kikubwa sana ukilinganisha na Matip na Lovren. Lakini waswahili husema ukiona Kilemba kimechafuka ujue kanzu haitamaniki.

Walio wengi walidhani kutoboka sana kwa safu ya ulinzi ya Liverpool shida ilikuwa Van Djik pekee.

Napingana sana na kauli za aina hii. Sio kweli kwamba safu ya ulinzi ya Liverpool imeimarika kwa sababu ya mtu mmoja pekee. Van Djik ni beki aliyekamilika kabisa. Yaani nampa asilimia 90 ya ukamilikaji wake. Ana msaada wa mkubwa sana kwenye timu. Unapokuwa na beki kama huyu unajua fika kuna kitu cha ziada kwenye safu yako:

Rekodi anazoshikilia Virgil van Dijk ndani ya Liverpool msimu huu:

πŸ”΄ Amegusa mpira mara nyingi zaidi (2,846)
——————————————————————–
πŸ”΄ Amecheza dakika nyingi zaidi (2,845)
———————————————————-
πŸ”΄ Amepigapasi nyingi zaidi (2,471)
————————————————————-
πŸ”΄ Amepokonya mpira mara nyingi zaidi (213)
———————————————————–
πŸ”΄ Ameokoa mipira ya hatari mara nyingi zaidi (173)
———————————————————-
πŸ”΄ Anaongoza kwa kuokoa mipira ya juu (155)
———————————————————–
πŸ”΄ Ametibua mipango mara nyingi zaidi (38)
————————————————————
πŸ”΄ Amezuia mashuti mara nyingi zaidi (13)
—————————————————————-

Ni kiongozi na ni mpambanaji pia. Van Djik ni beki anayefanya mabeki dhaifu waonekane bora (Gomez).

Lakini uwepo wake pekee sio sababu kubwa ya Liverpool kuwa imara. Zipo sababu nyingi sana. Labda tuanzie hapa kwenye ufanisi wa Liverpool mara baada ya usajili wake.

Orodha ya mechi ambazo Van Djik alicheza msimu ulioisha alipotua Liverpool akitokea Southampton

1/22/18 Liverpool FC Swansea City 1:0 CB L 90′
1/30/18 Liverpool FC Huddersfield Town 0:3 benchi
2/4/18 Liverpool FC Tottenham Hotspur 2:2 CB D 90′
2/11/18 Liverpool FC Southampton FC 0:2 CB W 90′
2/24/18 Liverpool FC West Ham United 4:1 CB W 90′
3/3/18 Liverpool FC Newcastle United 2:0 CB W 90′
3/10/18 Liverpool FC Manchester United 2:1 CB L 90′
3/17/18 Liverpool FC Watford FC 5:0 CB W 90′
3/31/18 Liverpool FC Crystal Palace 1:2 CB W 90′
4/7/18 Liverpool FC Everton FC 0:0 CB D 90′
4/14/18 Liverpool FC AFC Bournemouth 3:0 CB W 90′
4/21/18 Liverpool FC West Bromwich Albion 2:2 CB D 90′
4/28/18 Liverpool FC Stoke City 0:0 CB D 90′
5/6/18 Liverpool FC Chelsea FC 1:0 CB L 90′
5/13/18 Liverpool FC Brighton & Hove Albion 4:0 CB W 90′

MAELEZO: Msimu huu Liverpool mechi 19 wameruhusu magoli 7 tu na hawajafungwa mchezo wowote licha ya kutoka sare mechi 3. Msimu uliopita mechi 15 alizocheza Van Djik za mwisho kama chati inavyoonesha hapo juu Liverpool iliruhusu magoli 10, vichapo vitatu na sare 4.


Lakini safu ya ulinzi lazima iwe na muunganiko imara kutoka kwenye kiungo, mabeki wao kwa wao na kipa mwenye upeo mkubwa wa kuipanga safu yake. Tunaona chati hapo juu kuwa licha ya ujio wa Van djik katikati mwa msimu bado haukutibu tatizo lote.

Awali nimesema ukiona kilemba kimechafuka ujue na kanzu hali ni tete. Ukiona Timu inaruhusu sana magoli, shida ipo sehemu zote, mfumo, mabeki, viungo na kipa mwenyewe. Unaweza ukawa na kikosi imara na bora lakini mfumo ukasababisha timu iruhusu sana magoli (Real Madrid msimu uliopita)

Unaweza ukawa na kipa mbovu na mabeki wa kawaida lakini mfumo ukaisaidia timu kuzuia upenyo kuruhusu magoli mfano Barcelona haikuwa na kipa mzuri sana (Victor Valdes) ua Man United ya Mourinho ya msimu uliopita, haikuwa na mabeki bora sana lakini mfumo wake wa kuzuia sana uliifanya United kuruhusu magoli machache.

Mechi alizocheza Van Djik michuano ya Ulaya

Klabu vs.
2/14/18 Liverpool FC FC Porto 0:5 CB 90′
3/6/18 Liverpool FC FC Porto 0:0 benchi
4/4/18 Liverpool FC Manchester City 3:0 CB 90′
4/10/18 Liverpool FC Manchester City 1:2 CB 65′ 90′
4/24/18 Liverpool FC AS Roma 5:2 CB 90′
5/2/18 Liverpool FC AS Roma 4:2 CB 90′
5/26/18 Liverpool FC Real Madrid 3:1 CB 90′
Mechi 4 za mwisho tu waliruhusu magoli 10 Djik akiwemo

Sio ujio wa Djik pekee uliofanya Liverpool kuwa ngumu kufungika, ila ni mabadiliko ya mfumo (gegen pressing/mfumo wa kukimbia sana) na kucheza kwa tahadhari kubwa na kukaa na mpira. Pia usajili wa baadhi ya wachezaji muhimu kwenye maeneo ambayo yalikubwa na majanga. Ujio wa golikipa bora kabisa Becker Allison umefanya Liverpool kutokuruhusu magoli ya kizembe (Mignolet/Karius vs Bale).

Pia safu ya kiungo ilikuwa inachechemea sana. Wachezaji wengi hawakuwa na ubinifu sehemu hiyo. Tazama Henderson, Tazama Milner pia ugumu wa Emre Can. Ilikuwa mchezaji akiumia kwa upande wa Liverpool au akitepeta katika eneo hili hata Klopp nae alikuwa akitetemeka kwa sababu alijua wazi benchi hakuwa na kiungo mzuri zaidi ya yule aliyepo uwanjani.

Mchezaji pekee ambaye kidogo akionesha uimara wa hali juu kwenye sehemu hii ni Wijnaldum ambaye katika mechi 33 alizocheza msimu uliopita 21 tu ndio alicheza kwa dakika 90.

Ujio wa Naby Keita na Fabinho umemfanya Klopp achekelee sana. Sasa hivi anapata usingizi mororo kabisa kuelekea mchezo wowote kwa sababu anajua.

Ile tabia yao ya kukimbia kimbia ovyo kama kuku aliyekatwa shingo wameacha ndio maana wa acheza kwa utulivu mkubwa. Viungo wao ukitoa jiwe unaweka jiwe. Kipa bora kabisa, utulivu wa Van Djik umewafanya wengine kumuiga. Siri ya mafanikio ya Liverpool sio mtu mmoja kama wengi wanavyodhani. Unapokuwa na viungo wazuri wanaokaa sana na mpira kama Fabinho na Keita inapunguza adha kwa mabeki ya kukaba kaba ovyo. Mfumo wa kukimbia sana uliifanya Liverpool iwe na mabaka mabaka kwenye clean sheets zao.

Mechi 19 za mwanzo za msimu uliopita Liverpool ilifunga mabao matatu na kuendelea kwenye mechi 10, lakini msimu huu wamefanya hivyo mechi 7 pekee.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here