Home Kimataifa Sipo upande wa Shaffih wala upande wa Simba

Sipo upande wa Shaffih wala upande wa Simba

8857
1

Kumekuwa na kauli moja maarufu sana hapa nchini, “Anataka kututoa kwenye lengo” au “anataka kutuvuruga”. Hii kauli hutumiwa zaidi kuzuia watu kuisema Simba iwe kwa uzuri au ubaya. Manara hana makosa hata kidogo kuisifia klabu yake, hiyo ndio kazi yake. Lakini kuna mambo huwa siamini hata kidogo. Kuwanyima watu uhuru wa kusema wanayojisikia kuhusu Simba.

Manara na baadhi ya mashabiki wa Simba wanaamini kuwa ubora wa klabu yao utadumu kama klabu yao haitasemwa. Wanataka ipetiwepeitiwe, safi kila mtu lazima apende chake. Lakini msije mkaamini kwamba vilabu vikubwa ili vidumu havipaswi kusemwa.

Awali ya yote niwatoe hofu baadhi ya mashabiki wa soka wa Simba, kuwa treni haisimamishwi na honi ya baiskeli.

Simba wapo klabu bingwa hongera kwa hatua kubwa. Cha kusikitisha hawataki kabisa kusikia chochote kibaya kuhusu klabu yao. Iwe kweli au lah. Wao wanaamini piga ua alama 9 za hapa taifa lazima wazipate. Wana imani wanaweza baada ya kuwafunga Nkana FC.

Lakini kumtoa Nkana kusiwabweteshe!!. Nkana ni klabu ambayo iliwahi kuwa na mafanikio kiduchu klabu bingwa. Kwa sasa inajaribu kurudisha heshima mjini. Nkana FC naweza kusema ni sawa na Inter Milan ya sasa. Kiwango cha Simba labda tuseme kinakuwa kama KRC Genk. Genk ikimfunga Inter kufuzu UEFA haamaanishi kuwa kama atapangwa na Juventus na Atletico basi hilo kundi kwake nae atapewa nafasi kubwa kupita, kisa alimtoa Inter.

Simba yupo kundi gumu sana hapa naungana na Shaffih Dauda.

Wakati fulani inabidi ukweli usemwe ili ujue udhaifu wako na uutumie kama kigezo cha kupata unachokita.

Hivi mnataka tuwaambie kuwa Simba na AS Vital na Al Ahly mpo sawa? Uwekezaji wa Al Ahly kwa wachezaji kadhaa tu unatosha kuendesha ligi kuu bara miaka. Klabu ya Al Ahly ina thamani ya kikosi cha bilioni 78 za kitanzania. Sasa tukiwaambia ukweli mnapovukwa? Tazama chati hapo chini

No Klabu alama
1
Al Ahly – Egypt
1611
2
TP Mazembe – Congo DR
1595
3
Esperance – Tunisia
1583
4
Vita Club – Congo DR
1563
43
JS Saoura – Algeria
1475
Data hizi ni kwa mujibu wa footballdatabase
379
Simba SC – Tanzania
1247

 


Walio wengi ligi ya Afrika haitufuatilii ndio maana ni rahisi sana mtu kukwambia Simba na Vita wapo hadhi sawa. Huko ni sawa na kumpa nafasi Maccabi Haifa nafasi mbele ya Barca.


Vita sio timu ndogo. Vita imecheza mechi 45 ambapo imefungwa na timu za Congo mechi mbili tu [Mazembe 3-2 tarehe 4 mwezi wa 11, na kabla ya hapo ilifungwa miezi 8 iliyopita na Don bosco 0-2] Vita ilicheza takribani mechi 13 mfululizo bila kufungwa au kutoka sare ndani ya ligi kuu Congo kuanzia Tare 31/05 – 12/7 mwaka huu.

AS Vita iliwapiga wababe wa Simba Al Masry magoli 4. Mchezo wa fainali ya kombe la shirikisho dhidi ya Raja Cassablanca mchezo wa awali walifunga 3-0 Lakini wakiwa pale Congo Raja alikufa 3-1. Mashabiki wa Simba hata tukiwaambia hivyo tunawaharibia lengo?

Savio Kabugu beki wa SC Villa na timu ya taifa ya Uganda amesajiliwa na AS Vita

Wapo wengine wanadanganywa na baadhi ya taarifa ambazo hazijakamilika kwamba Al Ahly wapo vibaya kisa wapo nafasi ya 6. Kwanini hampendi kuchutama wakati wa mnavuliwa nguo? Al Ahly yupo nafasi ya 6 akiwa amecheza mechi ngapi?

Al Ahly amecheza mechi 12 tu na amefungwa michezo miwili akiwa na alama 24. Anayeongoza ligi Zamalek amecheza mechi 15 akiwa na alama 38. Waliopo juu ya Al Ahly wengi wao wao wamecheza mechi 18. Kama Al ahly atashinda viporo vyake vitatu atakwenda hadi nafasi ya 2. Al Ahly mwezi wa 10 walikumbwa na tatizo wakati kocha wao anaondoka. Mwaka huu mwezi wa 12 wameleta kocha mpya wa Uruguay Martín Lasarte na jahazi limetulia.

# M W D L G P
Zamalek SC 15 12 2 1 33:10 23 38
Pyramids FC 15 8 6 1 25:13 12 30
Masr El Makasa 17 8 3 6 19:15 4 27
Arab Contractors SC 16 8 2 6 23:16 7 26
Entag El Harby 18 6 8 4 19:18 1 26
El Ahly Cairo 12 7 3 2 18:9 9 24
Tala'ea El Gaish 18 6 6 6 25:22 3 24

Kumbuka wamemsajilia aliyekuwa kiungo bora wa ligi za Uarabun msimu uliopita.

El Shahata

Kiungo huyo anatokea klabu ya Al Ain waliocheza fainali ya klabu bingwa ya dunia na Madrid El-Shahat, kwa ada ya bilion 9 za Kitanzania. El-Shahata alicheza 33 akiwa Al Ain, nakufunga magoli 15 pamoja na assists 17.

Kiungo wa zamani wa Stock na Huddersfield Ramadhan Soby nae amarudi Al Ahly hivyo msiwapoze wenzenu kwa kuwadanganya Al alhy ya sasa ni mbovu. Tunaposema haya hatuwatishi, ila tunataka wajiandae katika hayo.

Simba nina uhakika kuna alama 6 kati ya 18 ambazo ana uwezekano mkubwa wa kupoteza. Shaffih amesema Simba ni Underdog na sio Favourite, ni kweli wala hakuna ubishi hapo. Vital 2014 walicheza fainali ya klabu bingwa, 2018 wamecheza fainali ya shirikisho. Al Ahly sina haja ya kuwaongelea sana. Hizi mechi mbili sina uhakika sana kama Simba anaweza kuambulia hapo alama 6 za ugenini.

Najua kwenye soka kuna kitu kinaitwa package of surprise. Na naamini katika hilo pia. Croatia kwenda fainali ya kombe la dunia, Korea kumfunga Ujerumani, Sweden kuwaondosha Italia, Leicester kutwaa ubingwa. Lakini package of surprise haiji kama miujiza. Ni Mipango thabiti na sio makelele. BVB 2013 waliushangaza ulimwengu wa soka kufika hadi fainali ya UEFA lakini haikuwa miujiza. Wale Wachezaji wao walikuwa na viwango maradufu.

Cassablanca vs vita fainali

Simba wasitarajie Package of Surprise kama hawajajiandaa kwa hilo. Package of surprise ni mipango, huwezi kutegemea package of surprise kwenye mechi 9, lazima ujiandae. Kujiandaa ni pamoja na kuyajua madhaifu yako. Madhaifu huwezi kutegemea akili yako pekee yako ndio maana wanazuka akina Dauda ambao wanaponda ili kuwatia hasira nyie mfanye kweli.


Mgema akisifiwa sana tembo hutia maji. Hatuwezi kutumia muda mwingi kuwapaka mafuta ilhali hatujawaambia mnawe.


Simba inapaswa kucheza kwa tahadhari kubwa sana. Kwanza wahakikishe Vita na Al Ahly mechi zote hawapotezi zaidi ya alama 4. Wahakikishe mechi zote hizo mbili hawakosi 4 kati ya 12. Utanishangaa sana kwanini. Vita na Al Ahly watakutana watachinjana, iwe sare au mmoja kushinda. Ili Simba isonge mbele pia wanapaswa kuhakikisha mechi yao dhidi ya JS Saoura hawakosi alama 3.5 yaani ushindi na sare.Kama watafungwa na mechi 3 za ugenini hapa nyumbani pia wanapaswa kushinda zote.

JS Saoura

Nimeona baadhi wakijaribu kuwachukulia kiurahisi hawa JS kisa tu wameanza 2008. Ndugu zangu wale JS hawana mchezaji ambaye thamani yake ni chini ya Euro milion 100, tena wachezaji ambao thamani yao ni ndogo ni

Thomas Ulimwengu
1993 (25) Tanzania
Seydouba Bissiri Camara
1995 (23) Guinea

Kikosi chao kina thamani ya hela za kitanzania bilioni 21.

Watu wanasema mpira una dunda, lakini haudundi wenyewe hadi udundishwe. Ukiwaambiwa umelogwa nenda kwa mganga kalogue au nenda kwa viongozi wa wakidini wakuombee na sio unalalamika tuna wivu. Hatuwachukii tunakumbusha.

Simba wanaweza kupindua matokeo lakini sio kwa kuwasifia au kuwatia moyo ila kwa kujipanga kisawasawa. Tusiwadanganyane kundi lao sio jepesi.

Comments

comments

1 COMMENT

  1. Priva Tambua Kuwa Mmbu ni Mdogo Sana lakin maumivu yake ni Machungu Sana. Hiv Pesa ndo Inacheza Mpira au Watu ndo wanacheza? Nahisi Msimu Ambao Leceister City wanachkua Kombe, ww Ulikuwa Darasa la Saba na Bado haukuanza Mchambua Mchele. Tatizo si Bajeti Kaka Badilika, Usiunge Mkono ujinga kisa Shaffih.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here