Home Kitaifa Star wa NDONDO CUP anafanya majaribio South Africa

Star wa NDONDO CUP anafanya majaribio South Africa

2399
0

Ukimuuliza Kelvin Sabato ‘Kiduku’ Kongwe (jezi namba 7 pichani) kuhusu safari yake ya soka lazima ataitaja Ndondo Cup. Ndio, ukipata fursa hiyo muulize ametokea wapi hadi kufika alipo sasa hivi.

Kiduku na wenzake ndio waanzilishi wa Ndondo Cup, alikuwepo msimu wa kwanza kabisa wa mashindano haya (2014) wakati huo alikuwa mchezaji wa Abajalo na aliisaidia kutwaa ubingwa wa msimu huo.

 

Ndondo kwake lilikuwa kama daraja (kumvusha kwenda ng’ambo ya pili), baada ya hapo alisajiliwa na Mwadui FC ya Shinyanga chini ya kocha Jamhuri Kihwelu ‘Julio’ wakati huo ilikuwa Ligi daraja la Kwanza Tanzania Bara, Kiduku akiwa katika msimu wa kwanza na timu hiyo akaisaidia kupanda Ligi Kuu Tanzania Bara.

Lengo lake la kucheza soka katika ngazi ya juu katika nchi hii likafanikiwa na alikuwa miongoni mwa wachezaji waliopanda na Mwadui hadi ligi kuu, kwake ikiwa ni mara ya kwanza kucheza ligi ya juu ya Tanzania.

Katika mishemishe za ligi kuu, Kiduku amechezea vilabu kadhaa kama Stand United, Majimaji FC na Mtibwa Sugar, huko kote moto wake unajulikana.

Kwa mara ya kwanza aliitwa timu ya taifa ‘Taifa Stars’ akiwa mchezaji wa Majimaji FC lakini leo Kiduku kuitwa timu ya taifa sio story tena ni jambo la kawaida.

Kwa sasa jamaa yupo zake Afrika Kusini akifanya majaribio ya wiki moja na Tshakhuma Tsha Madzivhandila Football Club (TTM F.C.) timu hii ipo katika Jimbo la Limpopo huko kwa Madiba.

Grafu yake inazidi kwenda juu, Ndondo Cup➡Ligi Daraja la Kwanza Tanzania Bara➡Ligi Kuu Tanzania Bara➡Timu ya Taifa➡Majaribio Afrika Kusini.

Wahenga walisema ‘Jasiri Haachi Asili’ tangu Kiduku ameanza kucheza Ndondo, kila msimu amekuwa akionekana katika mashindano hayo. Misimu miwili iliyopita alikuwa na Stim Tosha ‘Stamala’ chama la mtaani kwao Mabibo.

Kila la heri mwamba Kelvin Sabato ‘Kiduku’ Kongwe katika majaribio yako huko BONDENI.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here