Home Kimataifa Taarifa kuelekea mchezo wa Ufaransa Vs Ujerumani

Taarifa kuelekea mchezo wa Ufaransa Vs Ujerumani

10181
0

Lloris ataukosa mchezo wa leo na nafasi yake kuchukuliwa  na kipa wa Montpellier Benjamin Lecomte. Golikipa wa tatu wa PSG Areola, anatarajia kuanza mchezo wa leo dhidi ya Germany

Kocha wa Ujerumani Joachim Löw, amesema atawapa nafasi wachezaji wachanga na wale wenye uwezo. Na amethibitisha kuwa hana mpango wa kuongea na Ozil kuhusu uwezekano wa yeye kurudi timu yake ya taifa. Pia kocha huyo amewaongeza wachezaji kadhaa kikosini mchezaji wa Paris Saint-Germain Thilo Kehrer, na Nico Schulz wa Hoffenheim and na kinda wa Bayer Leverkusen Kai Havertz. Leroy Sane amerejeshwa tena kikosini.

Pia kocha mkuu wa Ufaransa Bwana Didier Deschamps amesema wao kubeba ubingwa wa dunia sio mzigo. Wamejiandaa kushindana na kupambana. Amesema yeye anapenda mechi za ushindani na hawezi kuibeza Ujerumani kwa sababu walitoka hatua ya makundi, bado anaamini kuwa ni timi bora. 

H2H

Katika michezo 29 iliyopita Ufaransa wameshinda mara 13, Ujerumani wakishinda michezo 9 na kutoka sare michezo 7. Ufaransa wamefanikiwa kuifunga Ujerumani mabao 47 na Ujerumani nao wamewafunga mabao 45.

Takwimu

Katika michezo mitano ya miwsho ya Ujerumani wameshinda michezo miwili na kufungwa michezo mitatu.

L KOR 2-0 GER 27 Jun, 2018 FIFA
W GER 2-1 SWE 23 Jun, 2018 FIFA
L GER 0-1 MEX 17 Jun, 2018 FIFA
W GER 2-1 KSA 8 Jun, 2018 kirafiki
L AUT 2-1 GER 2 Jun, 2018 kirafiki

Ufaransa imeshinda michezo minne na kutoka sare mchezo mmoja.

W FRA 4-2 CRO 15 Jul, 2018 FIFA
W FRA 1-0 BEL 10 Jul, 2018 FIFA
W URU 0-2 FRA 6 Jul, 2018 FIFA
W FRA 4-3 ARG 30 Jun, 2018 FIFA
D DEN 0-0 FRA 26 Jun, 2018 FIFA

Mara yao ya mwisho ya kukutana walitoka sare ya 2-2 novemba mwaka 2017.

Vikosi vinavyoweza kuanza.

Germany: Neuer (c) – Kimmich, Boateng, Hummels, Schulz – Gündogan, Kroos – Müller, Reus, Sane – Werner
Benchi: ter Stegen, Ginter, Kehrer, Rüdiger, Schultz, Süle, Tah, Brandt, Draxler, Goretzka, Havertz, Petersen
Kocha: Joachim Löw

France: Lloris (c) – Pavard, Varane, Umititi, Hernandez – Pogba, Kante – Mbappe, Griezmann, Matuidi – Giroud
Benchi: Costil, Areola, Rami, Sidibe, Mendy, Kimpembe, Tolisso, Nzonzi, Fekir, Dembele, Lemar, Thauvin
Kocha: Didier Deschamps

 


Wasimamizi wa mchezo huo

Mwamuzi

Daniele Orsato (ITA)

Waamuzi Wasaidizi wa golini

Lorenzo Manganelli (ITA)

Fabiano Preti (ITA)

Waamuzi wasaidizi

Marco Guida (ITA)

Daniele Doveri (ITA)

Kamisaa

Matteo Passeri (ITA)

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here