Home Kimataifa Taarifa za mrithi wa jezi ya Ronaldo tunazo

Taarifa za mrithi wa jezi ya Ronaldo tunazo

10636
0

Mshambuliaji mpya wa klabu ya Real Madrid, Mario Diaz, aliyetokea klabu ya Lyon, amepewa jezi namba 7 ambayo ilikuwa inavaliwa na Mshambuliaji wa zamani wa klabu hiyo Cristiano Ronaldo, alihamia klabu ya Juventus. Diaz, msimu uliopita ameichezea Lyon, michezo 45 na kufunga mabao 21.

Mariano
Taarifa Binafsi
Majina Mariano Díaz Mejía
Kuz 1 August 1993  (25)
Mah Premià de Mar, Spain
Kimo 1.82 m (6 ft 0 in)
Nafasi mshambuliaji

Diaz anasifika kwa nguvu na stamina uwezo wake wa kumilika mpira kwa ustadi mkubwa. Ana uwezo wa mashuti. Katika mabao 18 ya Lyon alifunga mabao 5 nje ya box la penati, hukua mabao manne akitumia jitihada na nguvu.

Ana kasi na ni mtulivu anapokuwa mbele ya lango. Anaweza asiwe mrithi sahihi wa Ronaldo lakini ni moja ya mwarobaini mzuri wa safu yao ya ushambuliaji. Katika mabao yake 18 amefunga penati moja tu wala hategemei faulo ila kasi yake na mashuti tu. Karimu Benzema ndani ya misimu mitatu iliyopita la liga amefunga mabao 18 wakati Diaz kafunga mabao hayo ndani ya msimu mmoja tu


Ronaldo mwenye umri wa miaka 33 alofunga mabao 450 katika michezo 438 akishinda La Liga mara mbili na   Copa del Reys mara mbili, Champions League mara 4. Ni ngumu sana kusema kuwa Mariano akiwa na umri wa miaka 25 anaweza kufanya aliyofanya Ronaldo.

Ronaldo akimkaba Diaz

Mariano pia alikuwepo kwenye kikosi kilichotwaa La Liga na Champions League mwaka 2016-17. Kabla ya kujiunga na Real Madrid alianzia maisha yake ya soka kule Espanayol.

Vijana
2002–2006 Espanyol
2006–2008 Premià
2008–2009 Sánchez Llibre
2009–2011 Badalona
2011–2012 Real Madrid

Mzaliwa huyu wa Premià de Mar, kule jijini Barcelona, Spain, alianzia maisha yake ya soka kule RCD Espanyol, kabla ya kwenda klabu ndogo ya CE Premià na kisha Fundaciò Sánchez Llibre. Mwaka 2009, alikwenda kujaribu bahati yake CF Badalona, na alicheza kikosi cha wakubwa  21 August 2011, akichukua nafasi ya Iñaki Goikoetxea huku akiishuhudia klabu yake ikitandikwa 1–0 kutoka kwa CD Teruel ligi Segunda daraja la B.

Timu ya wakubwa
Msimu Timu M M
2011 Badalona 3 (0)
2012–2014 Real Madrid C 46 (18)
2014–2016 Real Madrid B 44 (32)
2016–2017 Real Madrid 8 (1)
2017–2018 Lyon 48 (21)
2018– Real Madrid 0 (0)

 

Baada ya kujiunga na Real Madrid alikwenda kwenye akademi yao kabla hajapandishwa kikosi cha Castila.

Msimu wa 2014–15, akiwa na Castilla alicheza michezo 10 tu, 6 akitokea benchi, na kufanikiwa kufunga mabao matano. Kocha wa Real Madrid wakati huo Zinedine Zidane alimpandisha Mariano kikosi cha wakubwa 20 August 2016, baada ya Karim Benzema kupata na majeraha. Alifanikiwa kucheza mchezo wake wa kwanza Madrid wakiibuka na ushindi wa 2–1 walipokutana na Celta de Vigo, akichukua nafasi ya Álvaro Morata dakika ya 77.

Baadae  26 October, aliwafungia Merengues bao lake la kwanza kwenye kipigo cha 7–1 dhidi Deportiva Leonesa kwenye kombe la Copa del Rey. Alipewa nafasi tena kwenye mchezo wa marudiano ambapo alipiga hat trick yake ya kwanza kwenye ushindi wa idadi ya mabao 13–2. Mariano baadae alifunga tena mwenye ushindi wa 3–2 dhidi ya Deportivo de La Coruña. Baadae alitolewa kwa klabu ya Olympic Lyon kwa ada ya €8.

Mafanikio


Real Madrid:
La Liga: 2016–17
UEFA Champions League: 2016–17
UEFA Super Cup: 2016
FIFA Club World Cup: 2016


Hakuwa akitajwa tajwa sana licha ya kufunga mabao 18 ndani ya Ligue 1 huku akimzidi hata Mbappé. Mariano akishikilia rekodi ya kufunga bao kila baada ya dakika 43 kwa Madrid. Msimu wake wa mwisho alifunga mabao 25 ndani ya  Castilla akiwa anashikilia rekodi ya kuwa mfungaji pekee wa Castila kufunga mabao mengi ndani ya msimu mmoja.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here