Home Kitaifa Takwimu muhimu za Simba Vs TZ Prisons

Takwimu muhimu za Simba Vs TZ Prisons

12980
0

TZ Prisons

Tz Prisons katika mechi zake 6 za ufunguzi kafungwa mechi 2, Kashinda 3, na kasulu moja. Hii ni mara yake ya tatu kukutana na bingwa mtetezi.

Prisons imefunga mabao 6 na kuruhu mabao 6 ikiwemo kipigo cha mabao 3 kwa nunge kutoka kwa Ruvu Shooting.

Mara ya kwanza walikutana bingwa mtetezi ni msimu wa 2012/13 Alipokutana na Yanga na mchezo ulikwenda sare ya suluhu bin Suluhu

Mchezo wa Pili walikutana na Azam Fc

Mchezo ukaisha kwa Azam kuibuka na ushindi wa mabao 2-1.

Katika mechi zote 6 za mwanzo Prisons wameanzia ugenini mechi 5, wakishinda 3 na kufungwa mbili. Mechi pekee ya nyumbani walitoka sare ya bila kufungana na Yanga..

Simba SC

Simba haijwahi kupoteza mchezo wake wa ufunguzi katika mechi 6 zilizopita, ameshinda 4 na kutoka sare 2.

Simba imefanikiwa kufunga mabao 18 katika michezo 6 na kuruhusu mabao 5.

Wote katika michezo 6 wamefanikiwa kutoka michezo mitatu bila kuruhusu bao lolote na michezo mingine mitatu nyavu zao kutikiswa.

Msimu wa mwisho Simba imefanikiwa kufunga mabao mengi kuuizid Prisons. Simba imefunga mabao 62 na kufungwa 15 huku Prison ikifunga mabao 27 pekee na kufungwa mabao 22.

Msimu uliopita Prison ilishikilia nafasi ya 4 kwa kuruhusu mabao machache

Simba 15

Azam 16

Mtibwa 21

Prisons 22

Prisons ni timu ambayo ilionesha kuwa na ukuta mgumu sana.

Mchezo wa wa kwanza msimu uliopita kule Mbeya, Simba walipata ushindi wa bao 1-0 kabla ya kushinda bao 2-0 jijini Dar es Salaam.

16 Apr 18
Simba SC 2-0 Tanzania Prisons
18 Nov 17
 Tanzania Prisons 0-1 Simba SC
11 Feb 17
 Simba SC 3-0 Tanzania Prisons
09 Nov 16
Tanzania Prisons 2-1 Simba SC

Taarifa nyinginezo

Haruna Niyonzima inasemekana atarejea kambini kwa ajili ya msimu mpya.

Mohammed Rashid atapata wasaa wakukutana na timu yake ya zamani

Hassan Diluga kama atapata nafasi basi itakuwa mechi yake ya kwanza ya ligi akiwa na Simba

Meddie kagere, Paschal Wawa, Marcel, na chama utakuwa mchezo wao wa kwanza wakiwa na Simba.

Haji Manara maejigamba kuwachinja Prison hivi leo lakini klabu ya Prisons imesema haiwaogopi Simba kwani wao ni timu kma timu nyingine tu.
Kwa utabiri wangu sioni namna ya Prisons wataibuka na ushindi licha ya kwamba ni wabishi na wamekuwa wakicheza mpira mgumu sana. Wamepoteza Rashid na sioni namna wataweza kuipenya ngome ya Simba.
Simba 3-0 Prisons.
Utabiri wako ni upi?
Mimi ni Privaldinho.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here