Home Kitaifa “Tambwe ananikumbusha mbali”-Shaffih Dauda

“Tambwe ananikumbusha mbali”-Shaffih Dauda

4312
0

Jana Amis Tambwe alifunga hat-trick wakati Yanga ikishinda 4-0 dhidi ya Tukuyu Stars kwenye mchezo wa kombe la TFF (Azam Sports Federation Cup).

“Tambwe ananikumbusha kizazi cha washambuliaji ambao siku hizi siwaoni, washambuliaji ambao miaka fulani hivi walifunika sana kama Alan Shearer, Ruud van Nistelrooy, Marco van Basten, Michael Owen, Roy Makaay, David Trezeguet, Christian Vieri, mi-striker ambayo ina nguvu halafu inajua sana kufunga.”

“Tambwe hana papara halafu analijua goli kila angle, lakini sikuhizi kuna mabadiliko makubwa sana timu zinatumia mawinga watu kushambulia (Willian, Pedro na Hazard) wote wanacheza pembeni na wanaweza kuanza katika mechi moja. (Mahrez, Sterling na Sane) wakati mwingine wanaweza kuongoza mashambulizi.”

“Kumuona mshambuliaji wa aina ya Tambwe bado yupo na anafunga sio kitu cha kawaida kwa soka la kipindi hiki.”

Yanga imefanikiwa kufuzu hatua inayofuata ya Azam Sports Federation Cup baada ya kuitoa Tukuyu Stars katika mchezo wa jana.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here