Home Uncategorized Tanzania vs Afrika Kusini, Tukutane Coco Beach Jpili hii kuiunga mkono timu...

Tanzania vs Afrika Kusini, Tukutane Coco Beach Jpili hii kuiunga mkono timu yetu ya taifa

7474
0

Timu ya taifa ya Tanzania ya soka la ufukweni inaendelea na mazoezi kwa ajili ya kuikabili Afrika Kusini siku ya Jumapili kwenye uwanja wa Coco Beach kutafuta nafasi ya kufuzu AFCON upande wa soka la ufukweni.


Kocha msaidizi Ally Shariff Adolf ameeleza maandalizi yanavyoebdea hadi sasa.
:
“Timu yetu ipo katika maandalizi ya wiki ya nne kuelekea kwenye hiyo mechi siku ya Jumapili, tumemaliza program zote imebaki mambo madogomadogo kuelekea kwenye hiyo mechi.”


“Kikosi cha Tanzania cha mwaka huu kimetokana na mchanganyiko wa wachezaji wenye uzoefu ambao wamecheza mechi nyingi za kimataifa za Beach Soccer kutoka Zanzibar ambao wameungana na wenzao wa Tanzania bara waliocheza Copa Dar es Salaam.”

“Kikosi kipo vizuri sana na vijana wana ari kubwa, tunaomba watanzania wote waje watupe support siku ya Jumapili.”


Tukutane Jumapili COCO BEACH tunapigwa na upepo mwanana wa bahari huku tunapiga mihogo lakini tunapata burudani ya soka la ufukweni.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here