Home Kitaifa Tatizo ni maandalizi au soka letu linaongopa?

Tatizo ni maandalizi au soka letu linaongopa?

2558
0

Makala na Raphael Lucas
Katika mwaka ambao taifa la Tanzania lilikua na matumaini makubwa juu ya wawakilishi wao kimataifa kufanya vizuri ni msimu huu ambapo Simba sports club na wana tuliani Mtibwa sukari walikua wakiiwakilisha nchi katika mashindano ya kimataifa lakini mpaka sasa mambo si mazuri sana.

Safari ilianza kutiwa doa baada tu ya pale Mtibwa sukari kukumbana na kizingiti kikubwa kutoka kwa Waganda kilichosababisha kuondolewa kwenye hatua za awali na Waganda hao na hii ilionesha jinsi wenzetu walivyo sikiazi kwenye maandalizi yao tofauti na sisi, Tukaishia kusema tuwape mda Mtibwa kujifunza zaidi na kufanya maandalizi makubwa labda ipo siku watakuja kufanya vizuri zaidi.

Baada ya hapo safari ya matumaini ilibaki kwa Simba sports club hii ni baada ya kuwatoa vigogo wa soka kutoka ukanda wa kusini mwa Afrika Mbambane swallows na Nkana red devils kutoka Zambia na Simba kufuzu moja kwa moja kuingia kwenye hatua ya makundi ya klabu bingwa Afrika baada ya safari ya takribani miaka kumi na tano.

Haukupita mda mrefu makundi yakapangwa huko Cairo nchini Misri na Simba kuangukia kwenye kundi D likiwa na klabu za Al Ahly (Misri), As Vita (Congo DR),Js Saoura (Algeria) Pamoja na wawakilishi wetu Simba sports club. Safari ya Simba ilianza vizuri sana na kutia matumaini kiasi kufikilia juu ya kufika hadi hatua ya robo fainali hii ni baada ya kuwafurusha Waalgeria mabao matatu kwa nunge katika uwanja wa taifa pale kwa mchina ambapo waarabu hawanaga nafasi kubwa mbele ya Simba.

Kabla ya mchezo wa kwanza wa Simba wachambuzi wengi waliwachukulia Simba kama Underdog wa kundi hili akiwemo Shaffih Dauda na kupingwa na mashabiki na wanachama wa Simba hasa baada ya matokeo yao pale kwa mchina wakasahau safari ndo ilikua imeanza, Baada ya hapo Simba walisafiri mpaka Kongo kuwakabiri As Vita na kukutana na kibano cha fedheha toka kwa Wakongomani hao cha mabao matano pasipo kuambulia chochote, tukajua Simba wamejikwaa tu baada ya wiki moja wakasafiri mpaka kwa Waarabu ambapo katika kipindi cha kwanza tu Simba walikua washapokea kipindi cha magoli matano tena pasipo kitu.

Baada ya hapo watu ndipo wakaanza kuelewa maana ya neno Underdog ya Simba kwenye kundi lao, Pamoja na hayo sasa nagundua ni kwa hali gani soka letu linaongopa kuendana na hali halisi ya ushindani wake kisoka kwani Simba kwa mashindano ya Ndani wanafanya vizuri lakini kwenye uwakilishi wanashindwa kuhimilli mikiki mikiki, japo mpaka sasa kwenye makaratasi Simba wana nafasi kubwa kufuzu hatua inayofuata lakini kiuharisia ni vigumu sana.

“TFF hatukuhitaji ligi ya timu 20 kwa sasa pasipo na ushindani sahihi tulihitaji ligi ya timu 16 yenye ushindani sahihi”

Raphael Lucas (udom)
0710690782/0764764449


Picha zilizotumika ni nyota wa ndondo cup akadem Rabin Sanga anayefanya majaribio Besiktas ya Uturuki

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here