Home Kitaifa TFF’ maji ya betri yanafanana na maji lakini hayakati kiu

TFF’ maji ya betri yanafanana na maji lakini hayakati kiu

9025
0

Mimi: babu ameniuliza leo shida ya ligi kuu hasa ni nini mbona kama timu zipo nyingi na lile neno vodacom halionekani

(Babu yupo Rombo yeye mpira anauangalia kwenye TV hajui kinachoendelea huku mjini)

Nimemjibu babu huku mjini hali sio shwari. Kwanza timu zimeongezwa zipo 20.

Babu: kwani lile tatizo la umasikini limerekebishwa vipi?
Mimi: hali sio hali. Ligi kuu Tanzania bara haina mdhamini mkuu. Yupo mdhamini mwenza pekee.

Babu: mbona vilabu vingi ambavyo vimeshuka daraja vimelalamika kuwa hakuwa na uchumi imara imekuwaje sasa kama ligi haina mdhamini halafu bado mnaongeza vilabu?

Mimi: Babua unadhani najua basi?
Babu: unashindwaje kujua mjukuu wangu?
Mimi: Babu hawa TFF walijua kabisa mkataba wao na vodacom unaisha mwaka huu. Walitambua wazi msimu uliopita vilabu vikiyumba sana hasa kutokana na uchumi. Sjo klabu ndogo wala kubwa nyingi zililalama kuwa hali sio hali. Nashangaa TFF wakaongeza timu

Babu: Walisema sababu za kuongeza timu ni nini?
Mimi: Wanadai kuwa wachezaji wetu wanahitaji mechi nyingi?

Babu: Mechi nyingi huku watu wananjaa?
Mimi: Babu sijui, maana hata tatizo dogo tu kusimamia haki za waandishi wa habari imewashinda!
Babu: Kivipi?
Mimi: Hivi babu unajua mpaka sasa ID za waandishi wa habari kuingia uwanjani tu baadhi hazijatoka?
Babu: Kwanini
Mimi: Sijui labda mchakato wake ni mgumu ila Ndimbo amesema tusijali tutapa. Yaani inaonekana utaratibu wake ni sawa na wa kuagiza paspoti.
Babu: Kwahiyo mgawanyo wa mapato upoje?
Mimi: Kila mbuzi ale kwa urefu wa kamba yake
Babu: Unamaanisha nini?
Mimi: Kama una kijiwanja itakuwa kwako au kama huna mashabiki wa kutosha basi jiandae kutembeza kibakuli sokoni?

Babu: Sikuelewi
Mimi: mwenyeji ndiye atachukua mapato ya getini?

Bibi nae si akaingilia mazungumzo

Bibi: Looh! Vipi kuhusu hela ya mdhamini?
Mimi: Azam watazilipa vilabu vyote Milioni 162 ya matangazo ya TV na KCB watatoa Milioni 15 kwa kila klabu?

Shangazi: KCB ndio nani
Mjomba: Milion 15 dola au Yuro?
Mimi: Za kitanzania mjomba!
Babu: Ulisema timu zipo 20?
Mimi : Ndio babu
Babu: Yaani Milioni 15 ndiyo hela ya mdhamini kwa timu ambayo inatarajia kucheza michezo 38?

Shangazi: Kwani huyo KCB ndiyo mdhamini?
Mimi: Ndio, ila ni mdhamini mwenza
Babu: Kwahiyo Yanga yangu itakuwaje mjukuu wangu?
Mimi: Babu bora Yanga ina mashabiki wengi itatembeza kibakuli wataweza kumlia Fei toto ila timu hizi nyingine zilizoanzishwa kwa hela ya kibati ndio nazisikitia
Babu: Manji anarudi lini?
Mimi: Kwakuwa hakuaga atarudi kama alivyoondoka babu.

Mwisho wa siku TFF ijitathmini sana. Kuweka timu 20 na wakati uchumi ni tatizo kwa vilabu vyetu huku wakijua wazi hakuna udhamini wa uhakika ni ukanjanja tu.

Ni kweli klabu inapaswa kujitafutia mdhamini wake lakini ukweli ni kwamba asilimia kubwa vilabu vingi havina udhamini wa kueleweka.

Hata zile ambazo zina udhamini binafsi, bado fedha wanazopata hazitoshi kuzifanya zimudu gharama za kuendesha timu kwa msimu mzima wa ligi katika kusimamia masuala kama usafiri, huduma za malazi, chakula, posho na mishahara kwa wachezaji, makocha na watendaji wengine wa timu.

Unajiuliza wakati TFF wanapanga kuongeza timu mdhamini mkuu si alikuwepo kikaoni au walifanyia kikao sebuleni kwa mtu? Je kila klabu si ilikuwa na muwakilishi? Je kila mdau si anajua kiwa shida ya Tanzania ligi yetu kuna kudorora kwa uchumi? Je TFF haikujua kwamba msimu huu mkataba wao wa miaka mitatu na vodacom unaisha? Kwanini walikubali khingia kwenye mtego wa namna?

Kwanza kwa mawazo yangu wingi wa pua sio wingi wa makamasi. Eti ligi kuwa na timu nyingi ni sababu. Wekeni timu nyingi huko daraja la pili pia wekeni na mashindano mengi. Mnataka kucheza mechi nyingi ongezeni mzunguko wa makombe kama FA na kombe la Mapinduzi. Ratiba ya timu 16 tu tulisumbuana kwenye masuala ya viporo.

Kwanza kwa uchanga wa ligi yetu hatupaswi kuwa na timu 16 timu 12 tu zinatosha. Ni jambo la kushangaza sana. Nani alifanya huu utafiti? Alikuwa anawaza nini?

Nchi zenye uwezo mkubwa kama Afrika kusini ambao wana udhamini mnono zipo timu 16 sisi tulikuwa tunawaza nini?

Nchi ya Misri pamoja na utajiri wa mafuta wana timu 18 tu sisi tunataka kuonesha kitu gani?

Morocco na ujanja wao wote wana timu 16 pekee. Ndugu zao wa Tunisia wana timu 14 pekee mbali na kuzalisha timu bora kabisa kama Esperance. Aliyewaambia ubora wa ligi ni kuongeza timu? Wali haupikwi kwa moto mwingi ni taimingi ya moto.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here