Home Ligi EPL Tottenham Hotspur wanaweza amua hatima ya Mourinho, lakini United wanachekelea rekodi hizi

Tottenham Hotspur wanaweza amua hatima ya Mourinho, lakini United wanachekelea rekodi hizi

11293
0

Leo kuna Ndondo Cup Awards pale Clouds, mimi nitakuwepo. Na nina uhakika nitaangalia mechi ya United na Spurs kwenye laptop yangu kwa kuwa ninayo app ya DSTV , hivyo popote nitaangalia.

Okay sawa, ni hivi wakati Pep Gurdiola anajiunga na Manchester City watu waliamini mtu pekee ambaye anaweza kuwa mshindani wake ni Jose Mourinho kutokana na historia baina ya watu hao wawili.

Lakini baadae ikaanza kuonekana kama Mourinho na Pep ni watu wawili ambao wako dunia tofauti, huku Pep akiendelea kutawala soka na Mourinho akionekana kukwama.

Msimu huu wa EPL tangu mechi ya kwanza dhidi ya Leicester na kipigo kutoka kwa Brighton kumekuwa na mashambulizi mengi kwa Jose Mourinho kutoka kwa mashabiki, wachambuzi na wachezaji wa United wa zamani.

Michezo miwili ya mwanzo ambayo ilionekana mirahisi kwake imeibua mengi, na leo anakutana na mechi ambayo inaonekana ngumu kuliko mbili ambazo wamepitia.

Lakini hii ndio aina ya mechi ambayo Jose anaitaka kwa sasa, hii ndio aina ya mechi ambayo makocha wa kariba yake huwa wanaitumia kuinyamazisha dunia na kinyume cha hapo moto utawaka katika kazi yake.

Tottenham anaenda Old Traford leo wakiwa timu ambayo inaongoza kwa kufungwa katika uwanja wa Old Traford, wameshapigwa mara 21 katika safari zao kwenye uwanja huu.

Lakini Jose Mourinho anaweza kupata tumaini akikumbuka kwamba 1992/1993 ilikuwa mara ya mwisho kwa United kupoteza mara zaidi ya moja katika mechi zao 3 za ufunguzi.

Maurcio Pochettino ni kibonde wa Jose, kwani ameshafungwa mara 11 na Jose Mourinho na Pochettino hajawahi kufungwa na kocha mara nyingi kama alivyofungwa na Mourinho.

Toka mkesha wa mwaka mpya 2014 ambapo Tot waliifunga United, hakuna timu ya London ambayo imeshinda OT, kuanzia siku hiyo timu za London zilichukua alama 7 tu kati ya 66 Old Traford.

Lakini United watachekelea zaidi nkiwakumbusha kwamba katika mechi nne zilizopita kati yao na Tottenham hapa Old Traford, Manchester United walishinda mechi zotee.

Lipia 69,000 kwenye DSTV upate kifurushi cha compact na mechi hizi na nyinginezo utaziangalia live.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here