Home Kimataifa “Tukimfunga Man City kocha atimuliwe” Mashabiki wa Everton

“Tukimfunga Man City kocha atimuliwe” Mashabiki wa Everton

3938
0

Na Zaka za Kazi

Mashabiki wa Everton wangependa kuona timu yao ikipoteza mchezo wa leo dhidi ya Manchester City ili kuwakomoa wapinzani wao wa kitongoji kimoja, Liverpool FC.

Everton na Liverpool zinatoka kitongoji cha Merseyside kilichopo ndani ya jiji la Liverpool na upinzani wao wa kimtaa utawasababishia maisha magumu endapo Liverpool watakuwa mabingwa msimu huu.

Ili kuweka hali ya utulivu, wameitaka bodi ya klabu kumtimua kazi kocha wao, Marco Silva, endapo ataiongoza timu yao kuifunga Manchester City ambayo ndiyo timu pekee inayoweza kuizuia Liverpool isiwe Bingwa.

Mashabiki hao wametumia mtandao wa Twitter kutuma salamu hizo.

“Timua Silva endapo tutaifunga Man City Jumatano.” Aliandika shabiki mmoja, huku mwingine akiongeza: “Hebu dhania Marco Silva anashinda dhidi ya City, tutaondoka na kichwa chake.”

Wa tatu akasema: “Marco Silva amekuwa akipoteza kushoto, kulia na katikati. Naapa kumuua akiamua kubadilisha uelekeo huo dhidi ya City Juma hili”.

Mwingine ndo aliua kabisa: “Endapo Everton itaifunga Man City, afukuzwe Marco Silva…Endapo Chelsea itaifunga Man City, afukuzwe Sarri…suala hapa ni kulinda ubinadamu na utu kwa kuhakikisha [Liverpool] hawalisogolei kabisa taji la ubingwa wa Ligi Kuu.”

Kiasili wakazi wa mji wa Liverpool na wale wa mji wa Manchester ni mahasimu wa kihistoria lakini kelele za mbali hazikuzuii kulala kuliko kelele za karibu, kwa hiyo Everton wanaona bora City wawe mabingwa kuliko Liverpool.

Mwaka 2012, Liverpool walimfukuza kazi kocha wao Kenny Dalglish huku akiwa ameikifikisha timu hiyo fainali mbili; Kombe la FA na Capital One ambalo siku hizi linaitwa Carabao Cup. Moja ya sababu zilikuwa kukubali kumaliza ligi chini ya Everton.

Ni kosa kubwa sana kwa Liverpool kuwa chini ya Everton kwenye msimamo.

Kocha wao wa zamani, Bill Shankly, aliwahi kusema, ‘Ninapokosa kazi ya kufanya, naangalia msimamo wa ligi kuwaona Everton wanavyopambana na hali yao chini huko.’

Hii ndiyo kero ambayo Everton hawaitaki endapo Liverpool watakuwa mabingwa!

©Zaka za kazi

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here