Home Kimataifa “Tumeua sisimizi kwa nyundo”-Manara

“Tumeua sisimizi kwa nyundo”-Manara

5378
0

Baada ya ushindi wa Simba wa magoli 4-0 ugenini dhidi ya Mbabane Swallows kwenye michuano ya vilabi bingwa Afrika, afisa habari wa Simba Haji Manara amesema wametumia nyundo kuua sisimizi.”

Manara amesema Simba ilitumia nguvu nyingi kujiandaa na wapinzani wao jambo lililopelekea kupata ushindi mkubwa.

“Tulijipanga, unajua Mbabane kwa namna walivyocheza uwanja wa taifa walikuja vizuri sana kwa hiyo tulikuja kikamilifu.”

“Tunauzoefu nao kutokana na mechi waliyocheza dhidi ya Azam, wana mbinu chafu sana hasa nje ya uwanja, sisi tulikuja kamili tumejipanga.”

“Bahati mbaya tumetumia nyundo kuua sisimizi, kujipanga kwetu ndani na nje ya uwanja tukitufanya tutumie nguvu kubwa kiasi kwamba tumefanya mauaji makubwa. Tuliingia kwa tahadhali sasa hiyo tahadhali imemwangukia Mbabane.”

Simba imefanikiwa kusonga mbele baada ya kuisukuma nje ya mashindano Mbabane Swallows kwa ushindi wa jumla ya mabao 8-1.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here