Home Kitaifa Tuzo za heshima Ndondo Cup 2018

Tuzo za heshima Ndondo Cup 2018

5625
0

Kwa kutambua mchango wa wadau mbali mbali katika michuano ya Ndondo Cup 2018, usiku wa jana kulitolewa tuzo za heshima kwa baadhi ya wadau.

1.Wallace Karia. Raisi wa TFF Wallace Karia amekuwa moja ya watu ambao wanatuunga mkono sana, alikuwepo siku ya ufunguzi lakini hata siku ambazo hakuwepo alitusaidia kimawazo na kifikra katika michuano hii.

2.Mbwana Ally Samatta. Samatta amekuwa na Ndondo Cup tangu wakati inaanza na amekuwa karibia kila mechi za ufunguzi, huyu amekuwa balozi mzuri wa michuano hii ndani na nje ya nchi.

Hakuwepo usiku wa jana kutokana na majukumu aliyonayo katika klabu yake ya Genk haswa wakati huu wanapopambana kutafuta tiketi ya Europa lakini alipata wasaa wa kushukuru kupitia teknolojia ya video.

3.Afande Kombe. Ulinzi katika Ndondo ulikuwepo 100%, shukurani kwa jeshi la polisi ambao walihakikisha kila kitu kiko salama, Ndondo imeamua kumpa tuzo Afande Kombe kutokana na namna alivyopanga kikosi chake cha polisi kuhakikisha kila kitu kinakwenda sawa.

4.Daktari Kazi Ngongota. Daktari huyu tunamshukuru sana kutoka ndani ya uvungu wa mioyo yetu, kazi kubwa aliyoifanya kwa kujitolea katika michuano tangu tunaanza hatua ya makundi hadi kumaliza.

5.Yusuph Singo. Ukiacha Afande Kombe katika jeshi la polisi, kuna hawa Suma Jkt. Yusuph Singo alikuwa kiongozi wa Suma Jkt ambao achilia mbali kukaa getini katika mechi hizi walikuwepo wakati wote ndani ya uwanja kuhakikisha mashabiki wanakuwa salama.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here