Home Kimataifa Ubaguzi katika tennis, Black Panther yamchonganisha Serena Williams na French Open

Ubaguzi katika tennis, Black Panther yamchonganisha Serena Williams na French Open

13141
0

Serena Williams wakati anarejea katika michuano ya French Open mwaka huu ilikuwa habari kubwa, lakini habari nyingine ilikuwa ni nguo ambayo alivaa wakati wa mechi hizi.

Track Suit nyeusi ambayo ilikuwa na kama michirizi myekundu ilikuwa nguo ambayo ilitokana na movie maarufu ya Black Panther na ilikuwa ikivaliwa na mashujaa wa kike wa Wakanda.

Serena aliwahi kusema kwamba nguo hiyo ilikuwa ikimfanya kujihisi shujaa lakini vile vile alidai kwamba kutokana na kutoka kupata tabu wakati akijifungua, nguo hiyo inamfanya kujisikia fresh.

Serena anasema wakato akijifungua mtoto wake anaitwaye Olympia alipata matatizo makubwa katika mfumo wake wa mzunguko wa damu, na baadaye wataalamu walimshauri kuvaa nguo kama hiyo.

Bernard Giudicelli ambaye ni raisi wa French Open amesema katika michuano ijayo ya French Open sheria zitakuwa kali na watahakikisha hadi mavazi yawe wale wanayotaka wao.

Akizungumza na jarida la Tennis Magazine Bernard amesema kama vazi la Serena lilipitiliza na hawawezi kukubali mshindi huyo wa Grand Slam 23 kuvaa tena nguo hiyo katika michuano yao.

Watu wengi wameibuka mitandaoni ikiwemo waandishi wakubwa wa michezo na kuwashambulia French Open kwa kitendo hicho ambacho kinaonekana cha kibaguzi.

Ikumbukwe kwamba mwaka 1985 Anne White alishiriki michuano ya French Open na track kama ya Serena iliyofungiwa japo yake ilikuwa nyeupe na French Open hawakuizuia.

Wengi wanadai French Open hawaitaki nguo ya Serena kwa kuwa ipo katika movie ya kutetea haki za mtu mweusi, Serena bado hajatoa taarifa/jibu kutokana na kauli hiyo ya French Open.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here