Ubingwa wa Cosafa chini ya miaka 17 utuhamasishe ili tupige hatua zaidi.

  3875
  0

  Niipongeze timu yetu ya Taifa ya Tanzania ya Vijana chini ya miaka 17 SerengetiBoys, baada ya kufanikiwa kutwaa ubingwa wa mashindano ya Cosafa U17 yaliyofanyika Gaborone Botswana 2018

  Kutwaa Ubingwa inaonyesha ni kiasi gani vijana wameiva. Hakuna njia ya mkato kwenye mafanikio. Jambo pekee ambalo lililoshindikana kutekelezwa ni namna ya kuandaa kitu kama vile ni cha kesho. Mtoto umleavyo ndivyo akuavyo na pengine hawa vijana wetu chini ya miaka 17, bila shaka wanapitia misingi ya soka kuliko timu ya wale wakubwa. Hao vijana wa Serengetiboys wanakunjwa wakiwa bado wabichi.

  Tukifanya kitu ambacho ni endelevu na kuboresha miundombinu, tutapiga hatua kwenye sekta ya mpira wa miguu. Hakuna jambo lolote linaloshindikana. Tanzania ikiwa na vijana wengine hata 1000 ni matunda ya badae. Hata tukisubiri baada ya miaka 15 sio kesi. Kitu cha msingi ni kufikia lengo uliloliweka. Sio kitu rahisi kwenye swala la uwekezaji. Lazima uwepo muda wa kutosha na kuwa wavumilivu.

  Mipango ni mingi sana, kila siku unaweza kuamka ukiwa na mawazo mengi lakini tatizo ni maamuzi. Bila kuwa na watu wenye uelewa mkubwa wa soka, hakuna kinachoweza kufanyika.

  Hatuwezi kuongea kila siku bila vitendo.Vijana wa Serengeti boys wanazidi kutukurupusha tuamke mapema na mufanya maamuzi. Kabla ya kuwekeza vijana tuangalie kwanza tunawalea katika mazingira gani? Maandalizi ni muhimu zaidi kuliko kufikilia kukuza soka la Tanzania. Nina imani wale vijana wetu wa Serengeti boys hawatoshi kutufikisha pale tunapopaswa kuwa. Hakuna kitu kinachoweza kufanyika bila jitihada binafsi pamoja na kujituma. Kama nilivyosema, mandalizi yanapaswa kuanza kushika kasi kabla ya kufikiria mambo mengine. Bila kufanya hayo yote tutaishia kulalamika kila siku.

  Ujumbe kutoka kwa Patrick Admila

  Comments

  comments

  LEAVE A REPLY

  Please enter your comment!
  Please enter your name here