Home Kimataifa Uchambuzi: Atalanta Vs Juventus

Uchambuzi: Atalanta Vs Juventus

3766
0

Huu mchezo utachezwa katika dimba la Stadio Atleti Azzuri Bergamo, majira ya saa 17:00 kamili jioni. Atalanta, amepoteza michezo 64 ya ligi kuu Itali, dhidi ya Juventus, kuliko timu yoyote pia ukijumuisha michezo 23 kati ya michezo 27 waliyokutana na sare michezo 4.

Atalanta, ametoa sare katika michezo miwili ya ligi kuu ya mwisho dhidi ya Juventus, katika uwanja wa nyumbani kwa mabao 2-2 akiwa baada ya kupoteza michezo tisa ya nyuma dhidi ya Biancoheri, katika uwanja wa nyumbani. Tokea mwaka 2008 Juventus, wamefunga mabao 44 dhidi ya Atalanta, kuliko timu yoyote.

Atalanta, wamepoteza michezo mitatu kati ya michezo mitano ya mwisho kwenye ligi kuu ameshinda mara 2 akiwa baada ya kushinda michezo miwili kati ya michezo minne Kati ya minne iliyopita.

Juventus, wameshinda michezo minne ya mwisho katika ligi kuu katika viwanja vya ugenini pia kama katika mchezo huu wakishinda itakuwa rekodi ya kushinda michezo mingi ya ugenini msimu huu.

Juventus, katika michezo 27 katika ligi kuu dhidi ya Atalanta, ajapoteza mchezo hata moja ameshinda mara 23 na sare 4 akishikilia rekodi ya kushinda mchezo mingi dhidi ya timu moja ni Inter Milan, dhidi ya Sampodoria, Inter Milan, alishinda michezo 30 kuanzia mwaka 1961 mpaka mwaka 1977 ndo walicheza michezo mingi dhidi ya timu moja bila ya kupoteza.

Kama Juventus, watashinda mchezo huo basi watakuwa wamefikia rekodi yao waliyoiweka mwaka 2005-06 na mwaka 2013-14 kucheza mzunguko wa Kwanza na kufikisha alama 52.

Mchambuzi ni Azizi Mtambo 15

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here