Home Kimataifa UEFA Super Cup Atletico Madrid vs Real Madrid hii leo”moto hauzimi”

UEFA Super Cup Atletico Madrid vs Real Madrid hii leo”moto hauzimi”

8911
0

Kombe hili limeanzishwa mwaka 1972 na kuanza kutambulika rasmi mwaka 1973.

Kombe hili hukutanisha mshindi wa vilabu Bingwa barani ulaya na mshindi wa Ligi ya Europa

Klabu ya kwanza kutwaa kombe hili ilikuwa Ac Milan mnamo mwaka 1973 licha ya mwaka 1972 kufanyika fainali kati ya Ajax na Rangers ambayo haikutambuliwa na UEFA.

Hatimaye leo ndio ile fainali ya UEFA Super Cup ambapo bingwa wa Champions League Real Madrid atakuwa uwanjani kukabiliana na bingwa wa michuano ya Europa League Atletico Madrid.

Mchezo wa leo unaweza kuangaliwa kama jaribio kubwa la kwanza la kocha mpya wa Real Madrid Julen Lopetegui kuona namna anaweza kuibeba Real kama alivyofanya kocha aliyepita bila Cristiano Ronaldo.

Atletico Madrid wana sura mpya katika kikosi chao baada ya kumuongeza Thomas Lemar, Gelson Martin na Rodri japo wamempoteza nahodha wao Gabi pamoja Kevin Gameiro.

Thibaut Courtois aliyejiunga na Real Madrid akitokea Chelsea hatakuwepo langoni hii leo kwani bado hajakaa na timu kwa muda mrefu na anaweza josa match fitness lakini Kaylor Navas anaweza kuanza, huku kwa mara ya kwanza tangu 2009 Real wakicheza fainali kubwa huku Cr7 sio mchezaji wao.

Atletico Madrid wanaonekana wanyonge sana kwa Real Madrid katika michuano ya UEFA ambapo katika michezo 9 waliyokutana Atletico walipigwa mara 5, wakaumbulia suluhu 2, wakashinda mara 2.

Real Madrid katika mechi zao 6 za UEFA Super Cup walishinda michezo 4 huku fainali 2 za UEFA Super Cup zilizopita wameshinda na kama watashinda hii leo itakuwa timu ya kwanza kubeba kombe hilo mara 3 mfululizo.

Lakini leo inaweza kuwa tofauti kwani Atletico Madrid nao hawafanyagi kosa linapokuja suala la UEFA Super Cup, katika fainali zao 2 (2010,2012) wameshinda zote, 2010 wakiipiga Inter Milan 2-0, 2012 wakiipiga Chelsea 4-1.

Hii ni mara ya nne kati ya tano kwa fainali ya UEFA Super Cup kushirikisha timu za kutoka nchini Hispania lakini itakuwa mara ya kwanza kwa fainali hii kupigwa huku timu zikitokea mji mmoja.

Barcelona na Ac Milan ndivyo vilabu vilivyotwaa kombe hili mara nyingi zaidi (Mara 5 kila mmoja).

Hii ni kwa mara ya kwanza timu kutoka katika jiji moja kucheza katika fainali hizi.

Los Blancos ndio mabingwa wa kombe la UEFA super cup kwa msimu uliopita walitwaa baada ya kumfunga Manchester United 2-1.

Atletico Madrid wamefanikiwa kuingia fainali mbili na kutwaa kombe hili mwaka 2010 na Mwaka 2012.

Los Blancos wametwaa kombe hili mara 4 wanahitaji ushindi katika mechi ya Leo ili kuifikia rekodi ya Barcelona na Ac milan.

Usisahau kwamba mchezo huu unaweza kuuangalia katika simu yako na ni ukiwa na application ya DSTV pekee, cha kufanya lipia king’amuzi chako uweze kuuona mtanange huu live

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here