Home Ligi EPL Uhusiano wa Mo Salah na timu ya taifa Misri wazidi kuwa...

Uhusiano wa Mo Salah na timu ya taifa Misri wazidi kuwa pabaya, EFA waijibu barua yake

10371
0

Baada ya wiki iliyopita mchezaji wa Misri Mo Salah kuomba kupewa ulinzi wa juu kabisa na kuanza kupewa huduma za kipekee anapokuwa na timu ya taifa ya Misri, sasa chama cha soka nchini Misri (EFA) kimejibu mapigo.

Katika barua ambayo chama hicho cha soka nchini Misri wamemuandikia Salah wamemtaka asahau kuhusu madai yake kwani hakuna mchezaji anayeweza kupewa huduma tofauti na mwingine.

Misri wamesisitiza kwamba mchezo wa soka ni mchezo wa kitimu na sio nguvu ha mtu mmoja mmoja na ndio maana wao huduma zao kwa wachezaji wanazigawa sawa bila kubagua huyu ni nani na huyu ni nani.

“Kila mchezaji anayeteuliwa na chama cha soka/kocha kulitumikia taifa anahudumiwa sawa na mwenzake na heshima sawa, mchezo huu ni wa kitimu zaidi sio wa mtu binafsi” ilisema sehemh ya taarifa hiyo.

EFA wamepigilia zaidi msumari kuhusu tukio hilo kwa kusema kwamba hata namna walivyofudhu kwenda kombe la dunia haikuwa juhudi ya mtu mmoja bali ni timu nzima.

Rammy Abbas Issa ambaye ni wakili wa Mo Salah alikiandikia chama cha soka cha Misri barua hapo mwanzo akitaka Salah aongezewe ulinzi wa mabaunsa ambao watakuwa wanalala nje ya chumba chake akiwa kambini Misri.

Pia Rammy alitaka Misri waandae usafiri maalum ambao kila Salah akirudi Misri utakuwa ukimchukua kumpeleka hotelini, pia Salah asiwepo katika vyumba vya mahojiano ya timu ya taifa wala matukio ya wadhamini.

Sababu kubwa ya Rammy kutaka haya kwa mteja wake ni kile alichoita usumbufu kutoka kwa mashabiki, lakini sasa EFA (chama cha sola cha Misri) wamesema hilo ni gimu kufanyika.

Mvutano huu umeanza kuwakera watu nchini Misri kufikia hatua kuchana mabango yenye picha nyota huyo na kufuta picha zake kwenye kuta za mitaani, na haijafahamika nini Salah atafanya baada ya uamuzi wa EFA.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here