Home Kimataifa Ukistaajabu ya Kakolanya, utayaona ya Yondani

Ukistaajabu ya Kakolanya, utayaona ya Yondani

7776
0

Makala na Raphael LucasJina la Kocha mkuu wa kikosi cha wanajangwani, Dar es Salaam young Africans [Yanga] Papaa Mwinyi Zahera mtu ya Kongo limekua kwa kasi sana. Haliishi mdomoni mwa watu na media za Tanzania hii. Inatokana na misimamo yake hasa kwenye suala la nidhamu ya wachezaji wake. Hataki masikhara kabisa. Sio mtu wa kona kona.Mwishoni mwa mwaka 2018 kulitokea na kesheshe kubwa juu ya suala la aliyekua kipa namba moja wa kikosi hicho Beno Kakolanya. Kakolanya alitofautiana na kocha Zahera. Ni baada ya kugoma kujiunga na kikosi kutokana na matatizo ya kimaslahi. Kitendo kile kilemkera sana kocha Zahera. Kocha akamuondoa kwenye kikosi chake kwa kumuona kama msaliti.Wanachama walionesha jitihada za kumrudisha Beno kwenye kikosi cha wanajangwani kwa kumlipa shilingi milioni mbili za Kitanzania. Jambo hili lilipingwa vikali na Zahera. Zahera alionesha wazi na hamtaki tena Kakolanya.Muda mchache uliopita Zahera ametanganza kumvua kitambaa cha unahodha Kelvin Yondani. Na kumpa kitambaa hicho kiungo mshambuliaji Ibrahim Ajib. Yondani amevuliwa cheo kutokana na tabia zake za kuchelewa mazoezini.Namnukuu Zahera


“Niliwapa wachezaji siku tano za mapumziko ili siku ya sita waje mazoezini yeye hakutokea. Amezima simu na amegoma. Siwezi kumwacha mtu kama Yule anayepaswa kuonesha mfano kwa wengine afanye hayo hivyo nmeamua nimvue unahodha na kuanzia sasa nahodha ni Ibrahim’’Mwisho kumnukuu.


Ni ajabu mchezaji mkubwa kama Yondani kuzembea mazoezini, ilihali anajua misimamo ya Zahera. Najaribu kujiuuliza hivi kweli haoni jinsi Beno anavyosumbuka na huu msimamo wa Zahera? Amesahau kuwa yeye ni moja kati ya nembe muhimu Taifa stars.Wachezaji wengi wa kitanzania bado hawajakua kisoka. Wanafanya mambo ambayo hayaendani hadhi zao. Baadhi yao wamekosa ueledi na ukomavu kiakili.Pongezi zangu kwa Ibrahim Ajib. kuteuliwa kwake kuwa nahodha kumpe chachu ya kutaka mafanikio zaidi. Ikumbubwe nae amekuwa mara nyingi akiwekwa benchi na Zahera kutokana na masuala ya utovu wa nidhamu. Kwa sasa Ajibu anapaswa kuwa mfano wa kuigwa.‘’ZAHERA ENDELEA KUTUPA FUNZO WATANZANIA YA NINI MAANA YA NIDHAMU NA KUONGEZA UWELEDI’’Raphael Lucas [UDOM]0764764449/0710690782

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here