Home Kitaifa Ukweli kuhusu Manyika Jr kuvunja mkataba Singida United huu hapa

Ukweli kuhusu Manyika Jr kuvunja mkataba Singida United huu hapa

10909
0

Kumekuwa na taarifa kwamba klabu ya Singida United imevunja mkataba na golikipa Peter Manyika Jr kwa sababu haijamlipa mishahara ya miezi kadhaa.

Mkurugenzi wa klabu hiyo Festo Sanga amefafanua jambo hilo.

“Hatuna taarifa yoyote ile kwamba mkataba wa mchezaji wetu Peter Manyika kwamba mkataba wake umevunjika. Mimi ndio mtendaji mkuu wa klabu kwa hiyo ningepata taarifa na kwa ushirikiano ambao viongozi tunao tungefahamishana.

“Manyika ni mchezaji wetu tumemsajili kwa mkata wa miaka miwili, mkataba wa mwaka mmoja umeisha na hatudai chochote kwenye huo mkataba. Kilichobaki ni mkataba huu wa pili ambao umeanza kufanya kazi baada ya ligi kuanza August 22, 2018.”

“Manyika hayupo kambini kwa kipindi hiki kutokana na sababu ambazo Singida United na baba yake tunazifahamu na tulikubaliana. Manyika tunamtegemea atajiunga na timu.”

“Kama kuna hilo jambo, tunaamini mchezaji anatambua taratibu zinazofuatwa au kama kuna kiongozi wake anamsemea atambue kuna taratibu.”

“Kama klabu hatuna tatizo na Manyika na tunamtegemea ajiunge na timu muda wowote kwa hiyo Manyika ni mchezaji wa Singida United amebakiza mkataba wa mwaka mmoja kama kuna taarifa nyingine tutazitolea ufafanuzi.”

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here