Home Kitaifa Ulimwengu vs Simba kwa mara ya kwanza

Ulimwengu vs Simba kwa mara ya kwanza

5422
0

Baada ya draw ya makundi ya vilabu bingwa Afrika Simba imepangwa Kundi D ambapo ipo pia timu iliyomsajili mshambuliaji wa Tanzania Thomas Ulimwengu ‘Buffalo’ .

Unaweza kuona kama maajabu lakini ndivyo ilivyo, story kubwa si Thomas Ulimwengu kukutana na Simba lakini story kubwa ni Ulimwengu kucheza dhidi ya Simba kwa mara ya kwanza!!

“Katika maisha yangu ya soka, sijawahi kucheza mechi dhidi ya Simba kwa hiyo ni kitu kikubwa kwangu. Sio tu kwamba nakutana na timu kutoka taifa langu ila utakuwa ni mchezo wangu wa kwanza dhidi ya Simba”-anasema Ulimwengu.

“Timu zote ni ngumu kwenye kundi, naziheshimu timu zote. Simba ni timu nzuri hadi imefanikiwa kufika hatua ya makundi imedhihirisha kwamba ni timu nzuri.”

AS Vita ni timu ambayo Ulimwengu anauzoefu nayo kwa sababu ameshacheza nayo mara nyingi wakati akiwa TP Mazembe. Al Ahly amecheza nayo pia mara nyingi katika michuano ya mabingwa Afrika akiwa Mazembe vilevile.

Watu wengi walikuwa wanatarajia kwa kuwa Ulimwengu ni mtanzania na Simba inatoka Tanzania basi atakuwa amewahi kukutana nayo.

Amesema timu yao ni nzuri, ina wachezaji wawili ambao hawana asili ya kiarabu (raia wa Senegal na yeye) ni timu yenye ushindani mkubwa na bosi wa timu amewekeza ili timu ifanye vizuri.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here