Home Ligi EPL Unai atamuua Ozil kwa mwendo huu

Unai atamuua Ozil kwa mwendo huu

5797
0

Mezut Ozil, anapiga pasi kulia anapokea maelekezo kushoto. Ozil ni mmoja kati ya viungo namba 10 bora duniani. Anacheza taratibu sana utadhani kinyonga, lakini maamuzi yake hufanya mpira kuondoka mguuni mwake kwa kasi ya ajabu.

Upeo wake, welendi wake, utundu wake unamfanya awe mbunifu kwenye suala la upigaji pasi konki.

Mfumo wake wa mwili ni tofauti sana na muunda wa soka la Unai Emery.

Sio kwamba Unai anamchukia, sjui maana sipo moyoni mwake, lakini kinachoonekana ni kwamba, Ozil sio kikombe chake chai. Unai anapoamka asubuhi anawaza kuhusu wachezaji wengine 23 kuliko Ozil ambaye yeye anaona hamfai.


Unai ameomba radhi mashabiki wa Brighton baada ya kupiga chupa teke ambayo ilimlenga shabiki mmoja wakati timu yake ikitoka sare dhidi ya Brighton


Nadhani wengi mnakumbuka sakata la Arda Turan kutoa kauli ngumu sana wakati anaondoka Atletico, “Siwezi kukimbia ovyo kama Mbwa”

Soka la Unai linamfanano fulani kimazoezi na lile la Diego Simeoni, na yule Jurgen klopp wa miaka 7 iliyopita. Unakumbuka vyema Klopp alipotua Liverpool na ile gegen pressing yake? Kila wikiendi lazima usikie wachezaji wanaumwa misuli.


Taarifa mbalimbali zinadai Emery Unai amewaambia mabosi wa Arsenal wahakikishe wanamsajili kiungo Muargentine Ever Banega anayekipiga kunako klabu ya Sevilla


Pia ili tuende sawa, hivi majuzi wakati Unai anasajiliwa mwanzoni kuna video zilisambaa sana zikionesha wachezaji wa Arsenal walivyokuwa hoi kwa mazoezi makali?

Kuna mambo mengi hapa yanamfanya Ozil anakomba mboga kuliko wenzake lakini akifika uwanjani anawategea. Mesut Ozil ndiye anayeongoza Arsenal kwa kulipwa na ndiye mchezaji namba 2 England kwa mshahara mnono.

 1. Alexis Sanchez: £315,000 kwa wiki ($21.5M kwa mwaka)
 2. Mesut Özil: £306,250 wiki ($20.9M kwa mwaka)
 3. Paul Pogba: £290,000 kwa wiki ($19.8M kwa mwaka)
 4. Kevin De Bruyne: £280,000 kwa wiki ($19.1M kwa mwaka ) …
 5. Romelu Lukaku : £250,000 wiki ($17.1M kwa mwaka) chanzo CNBC
 • Ozil alicheza chini ya Mou lakini kiwango chake kilikuwa kizuri. Ninachoamini kila dereva ana ujuzi wake na barabara zake. Kwa Unai Ozil haoni kama anamfaa sana.


  Mesut Ozil Chini ya Mourinho

  2011: Mabao 10 assists 29
  2012: Mabao 7 assists 29
  2013: Mabao 10 assists 24

  Ozil chini ya Wenger
  2014: Magoli 7 Assists 14
  2015: Magoli 5 assists 7
  2016: Magoli 8 assists 20
  2017: Magoli 12 asissts 14
  2018: Magoli 5 assists 14


  Chati hapo juu pia inaonesha ni kwa namna gani mabadiliko ya kimbinu na mfumo yalimfanya Ozil aonekana mzuri hata katika Madrid ambayo kocha wake alipenda sana mpira wa kukaba

  Ozil sio kwamba ni mbovu, hapana, ila mwalimu hataki kujenga mfumo mpya kutokana na wachezaji aliowakuta ila anataka kuwajenga wachezaji katika mfumo anaoutaka yeye.

  Hii ni hatari sana, labda kama atapewa hela ya kufanya usajili. Mtu kama Ramsey anataka kuondoka, Ozil huyu pia ana wazo hilo hilo la kuondoka. Sio mbaya sana licha ya kwamba tunaona mfumo wa Unai umekubali kwa kiasi fulani. Timu inacheza soka safi na la kueleweka.


  Baadhi tu ya wachezaji ndio wanaonekana kuyumba kama Ozil, Ramsey na Mkhitaryan wanaonekana kutokwenda sawa na kasi ya Unai. Nadhani kuna mawili, Unai amruhusu Ozil kuondoka au azidi kumwacha Ozil atengeneze makundi ndani ya klabu. Mara nyingi nyota kama hawa wakicheza kwa kushinikizwa majukumu au kuachwa benchi sana au kutolewa ovyo kama mechi yao dhidi ya Brighton kuna hatari kubwa sana.

  Yote kwa yote Unai ni mwalimu mzuri sidhani kama atakosa namna ya kumtumia Ozil na kama akishindwa sio Ozil amefeli ila yeye mwenyewe.

  Comments

  comments

  LEAVE A REPLY

  Please enter your comment!
  Please enter your name here