Home Kitaifa Unakosaje show ya Serengeti Boys?

Unakosaje show ya Serengeti Boys?

8241
0

Kocha mkuu wa Serengeti Boys Oscar Mirambo amewaomba mashabiki wa soka kutoka maeneo mbalimbali kwenda kuiunga mkono timu ya taifa ya vijana chini ya miaka 17 itakapokuwa inacheza mechi yake dhidi ya Rwanda.

Serengeti Boys leo itacheza mechi hiyo huku wakiwa vinara wa Kundi A wakiwa hawajapoteza katika mechi mbili walizocheza hadi sasa katika kuwania kucheza fainali za Afrika mwaka ujao.

“Nitumie nafasi hii kuwaomba watanzania wenzetu wajitokeze kwa wingi uwanjani ili kuwapa hamasa vijana lakini pia kuangalia timu imefika wapi pamoja na changamoto za kutatua kabla hatujafika AFCON mwakani.”

“Timu yetu ni timu pekee ambayo ina malengo tofauti na timu zote ambazo zipo kwenye haya mashindano. Wote tunafahamu, timu zote zinatumia mashindano haya kwa ajili ya kutafuta nafasi ya kufuzu kwenda AFCON 2019 ambapo Tanzania tutakuwa wenyeji.”

“Kwetu sisi ni tofauti, tunatumia mashindano haya kama sehemu ya kuangalia tumefikia wapi kwenye maandalizi ya timu yetu na changamoto gani ambazo tunatakiwa kuendelea kuzitatua kabla ya kufika 2019 ambapo tutacheza AFCON.”

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here