Home Uncategorized Underdog watafunwa kwenye Derby ya Watanzania

Underdog watafunwa kwenye Derby ya Watanzania

3729
0

Kule nchini Kenya leo kulichezeka Derby ya watanzania wawili, Aman Kyata (Nakumatt FC/Mt Kenya United) dhidi ya Hamis Abdala wa Bandari FC.

Mchezo umekwisha kwa Mt Kenya wanaoshikilia mkia kufungwa FC 2-1 wakiwa nyumbani.

Mt Kenya wanaoshikilia mkia walipambana kujaribu kuwazuia Bandari walimaliza nafasi ya pili msimu uliopita. Hata hivyo katika mtanange huo wa kukata na shoka, Aman Kyata hakujumuishwa kikosini kutokana na majeraha.

Kwa matokeo hayo Bandari FC kufikia sasa wana alama 15 nyuma ya Mathare United wenye alama 17 wote baada ya kucheza michezo 7.

Mt Kenya anayochezea Aman Kyata ipo mkiani ikiwa na alama mbili ikiwa haijashinda mchezo wowote. Kyata alijiunga na Mt Kenya maarufu Nakumatt baada ya kukamilika kwa msimu uliopita.

Klabu anayochezea Jamal Mwambeleko KCB nayo ilitoa dozi ya goli 1 ugenini dhidi ya FC Leopard

Nyota wa zamani wa kimataifa wa Kenya Denis Oliech aliyesajiliwa na Gor Mahia hivi majuzi aliisaidia klabu yake kupata alama 10. Gor Mahia wapo nafasi ya 6w akiwa wamecheza michezo 6.


Matokeo mengine

Saturday SPL results

Tusker FC 1-2 Mathare United

Mt Kenya United 1-2 Bandari FC

AFC Leopards 0-1 KCB FC

Kakamega Homeboyz 1-1 Zoo FC


Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here