Home Kimataifa United sio sehemu sahihi kwa Pochettino

United sio sehemu sahihi kwa Pochettino

4487
0

Manchester United, ni moja ya timu kubwa duniani kwa ujumla ina kila aina ya mataji timu hiyo iliyoshiriki hakuna mtu asiyejua ukubwa wa klabu hiyo ukiwa mfuatuliaji wa mchezo wa soka kipindi cha miaka ya nyuma ukisikia jina la klabu hiyo ni lazima uogope kuanzia nje ya uwanja mpaka ndani ya uwanja kwa maana ya kupata matokeo mazuri.


Nadhani Pochettino anafuraha pale Spurs sioni sababu ya yeye kwenda pengine” Unai Emery


Tukumbuke klabu hiyo tangu alipostafuu kocha mwenye heshima yake babu Sir Alex Ferguson, msimu wa mwisho wa mwaka 2011-12 wakitwaa taji la ligi kuu England hakuna kocha hata moja aliyetwaa taji hilo tena?sasa imepita miaka 6 bila ya taji hilo kweli maisha yanaenda kasi tulizoea kila msimu Manchester United, kama aitwaa taji basi itamaliza nafasi ya pili na msimu ujao watwaa taji hilo.

Tangu alivostafuu Babu Ferguson, hakuna kocha aliyetwaa mataji zaidi ya Jose Mourinho, tena msimu wake wa Kwanza mwaka 2016 pengine wapo watu waliamini kuwa uzoefu wa Jose angeleta mabadiliko lakini mambo yameenda ndivyo sivyo katika klabu hiyo kuna vitu vinaendelea embu tuachane na hayo.


Kuna timu kama Spurs na kuna timu kubwa ambayo ni United. Pochettino ana hadhi ya kuwa klabu kubwa” Jap Stam


Baada ya kufutwa kazi Jose, nimeona watu wengi wakimpa nafasi kocha wa klabu ya Tottenham Hotspur, Mauricio Pochettino, kuvaa viatu hivyo?

Nilijiuliza mara mbili Pochettino, ataiweza kweli Manchester United? Sio mwalimu mbovu ni mwalimu mzuri lakini Manchester United, timu yenye presha Kiowa zaidi kwa maana kila msimu wanataka wafanye vizuri na kutwaa mataji kama zilivokuwa enzi za Ferguson hata ukiangalia Tottenham, na Manchester United, ni timu mbili tofauti.

Tottenham ni timu ambayo aina presha katika ligi kuu kwa maana ya kutwaa mataji itoke tu labda watwaa taji kama ilivokuwa klabu ya Leicester City msimu ule? hakuna mwana michezo atakaeuliza kwa nini Tottenham, ashindi mataji ni wachache sana pengine ndo hata Pochettino hana presha kubwa Spurs, akishiriki michuano ya Uefa ni faraja kubwa kwao.


Mourinho kwa siku 895 alizoishi katika hoteli ya The Lowry hotel kule Salford aliigharimu United £537,000.


Tumewaona makocha ambao wamepita Utd, David Moyes, alikuwa kocha mzuri wakati yupo Everton, lakini alivoenda Manchester United, alishindwa kuwapa kile kitu ambacho Utd walikuwa wanakiitaji.

Manchester United, wanahitaji watafute kocha mwenye CV kubwa ambaye ana mafanikio na uzoefu atakayeweza kuja kuleta ushindani mbele ya Pep, Klopp, Sarri.


Kocha wa Real Madrid Santiago Solari amesema hatishwi na taarifa na Mourinho kuhusishwa na kuchukua kibarua chake Bernabeu


Soko la makocha limekuwa gumu sana kwa sababu kila kocha yupo katika timu husika njia mbadala na kuvunja mkataba.

Hayo ni mawazo ya Aziz Mtambo

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here