Home Kimataifa United yasaka mkurugenzi, De gea mkataba mpya, Silva abwaga manyanga

United yasaka mkurugenzi, De gea mkataba mpya, Silva abwaga manyanga

10929
0

Manchester United wameanza mchakato wa awali wa kutafuta Mkurugenzi wa Michezo kwa mara ya kwanza katika Historia ya Klabu hiyo huku Golikipa za zamani wa klabu hiyo Edwin van der Sar na Mkurugenzi wa Michezo wa sasa wa AS Roma Monchi ndio wanapewa nafasi kubwa. Matatizo yaliyotokea katika dirisha la usajili la majira haya ya kiangazi yapelekea Man United kutaka kubadilisha mfumo wao wa idara ya usajili , kitu ambacho kiliwahi kupendekezwa miaka miwili iliyopita.
Golikipa wa zamani wa Man United Van der Sar anapewa nafasi kubwa kutokana na mahusiano yake na klabu hiyo lakini pia na kazi nzuri ambayo mpaka sasa ameifanya ndani ya klabu ya Ajax. Mkurugenzi wa Michezo wa Roma Monchi na yule wa Juventus Fabio Paratici nao wanawindwa kwa karibu na Mtendaji Mkuu wa United , Ed Woodward. Mkurugenzi wa Michezo mpya atafanya kazi kwa karibu sana na timu ya idara ya usajili ya sasa ya United ambayo ipo chini ya Ed Woodward na Jose Mourinho . Kazi kubwa itakuwa kuhakikisha United wanakuwa na mipango ya muda mrefu ili kuondoa purukushani za kufanya usajili dakika za mwisho za dirisha la usajili.

Beki wa kati wa Bayern Munich, Jerome Boateng anaweza kujiunga na Paris St- Germain ikiwa makubaliano yatafikiwa baina ya ya klabu hizo

Klabu ya Manchester United, inatarajia kumpa mkataba mpya kipa David De Gea ambao utamfanya alipwe paundi 200,000 kwa wiki

Kiungo mchezaji wa manchester City David Silva ametangaza kustaafu Soka LA kimataifa. Kiungo huyo Wa Uhispania aliwaandikia mashabiki Barua ya kuwaaga baada ya kucheza michezo 125 kwa nchi yake. Mchezaji Huyo mwenye miaka 32- aliongea na kocha wake Man City Pep Guardiola juu ya namna bora ya kuweka ratiba take vizuri ili aweze kupata muda mzuri ili aweze kuwa karibu na mwanae wa kiume aitwaye Mateo mwenye umri Wa miezi saba. Mtoto huyo alizaliwa kabla ya muda(njiti) mwezi Desemba mwaka uliopita na kukaa miezi mitano akiwa hospitali ya Valencia’s Casa de Salud.

Klabu Psg inaandaa paundi milion 100, kwaajili ya kupata saini ya kiungo mchezeshaji wa Tottenham Christian Ericksen

Beki wa kulia wa Manchester United Matteo Darmian, anataka kuondoka Old trafford, huku Vilabu vya Napoli, Inter Millan na Juventus vikihusishwa kumsajili mlinzi huyo, mwenye umri wa miaka 28 .

Winga wa Crystal Palace Wilfried Zaha, anajiandaa kusaini mkataba mpya ili kuendelea kuichezea timu hiyo

Kiungo wa Klabu ya Chelsea, Reuben Loftus Cheek anatarajia kujiunga na Borussia Dortmund kwa mkopo wa mwaka mmoja. Kocha Maurizio Sarri, hakumpanga kwenye mechi ya juzi dhidi ya Huddersfield town, na pia ujio wa kiungo Mateo Kovacic umefanya kiungo Loftus Cheek, asiwe na uhakika wa kucheza mechi nyingi za msimu huu.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here