Home Ligi Uongozi wa Alliance watoa rai kwa mashabiki wote

Uongozi wa Alliance watoa rai kwa mashabiki wote

8021
0

Baada ya Alliance kupoteza pambano lao la jana dhidi ya Prisons ya Mbeya mashabiki wengi wa klabu hiyo na wengineo wamekosa uvumivu na kiwango cha timu hiyo na kuamua kwenda kutukana kwenye ukurasa wao wa Instagram.

“Naomba niwaambie jambo ambalo watu wengi huwa hawaelewi na kama wanaelewa basi wanafanya makusudi, mpira wa miguu una matokeo matatu kushinda, kushindwa na kutoka sare”

Uongozi huo bado una matumaini na kikosi chao na kupoteza michezo miwili kati ya mitatu ya awali sio sababu kubws ya kukata

“Sisi kama timu tumeanza ligi na tumecheza michezo mitatu tumetoka sare mchezo mmoja, tumefungwa miwili na ukiangalia siyo matokeo mabaya kiasi hicho hadi kufikia kunyosheana vidole”

Licha ya wao kudhihakiwa kuwa wanatumia wanafunzi bado kikosi chao ni imara

“Sisi kama uongozi tunaimani kubwa na benchi la ufundi, wachezaji na tunamshikamano wa hali ya juu na tuna morali kubwa huku tukiamini tutafanya mambo makubwa ambayo wengi wenu hamtakaa na kuamini”

“Tumebakiza michezo 35 na tunaomba kwa kipindi hiki ambacho tunakipitia ninyi wadau wetu na mashabiki wetu mtuunge mkono na tushikamane sote lakini pia hiki ni kipindi cha kukaa na kutulia huku tukitafakari nini kifanyike kwenye michezo inayofata.”

Pia ameendelea kuwaasa wachezaji wao kutokukatishwa tamaa na mambo ya nje

“Nafahamu kuwa mtaitwa kila aina ya majina, mtatukanwa sana na watawapa maneno ya kuwa katisha tamaa sana lakini ndugu zanguni safari bado tena bado saana na hakuna timu inayofahamu mwisho wa safari yake zaidi ya MUNGU pekee”

Siku zote huwa nasema sisi tupo tofauti na utofauti huo tunauonesha hata tukifungwa bado tunaweka matokeo yetu kwani huo ndiyo mpira na tusiwe tunaweka tunayoshinda tuu au yanayo furahisha pekee bali hata yanayo umiza yawe yanawekwa na tutaendelea kufanya hivyo kwa kila mchezo tunao ucheza.

Pia alitoa rai kwa mashabiki

“Mwisho ningewaomba tusitumie ukurasa huu kutukanana na kudhihakiana bali tushauriane na tupeane mbinu za kufanya tufanikiwe”

Imetolewa na mkuu wa habari na mawasiliano Alliance Fc

Jackson Luka Mwafulango
02.09.2018

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here