Home Ligi BUNDESLIGA Usajili wa Pogba kwenda Ujerumani wakwama sababu ya unene

Usajili wa Pogba kwenda Ujerumani wakwama sababu ya unene

13307
0

Kaka mkubwa wa Paul Pogba aitwaye Mathias Pogba amekataliwa kucheza soka nchini Ujerumani katika klabu ya KFC Uerdingen kutokana na uzito uliopitiliza.

Mathias alikuwa ni mchezaji huru baada ya kutemwa na klabu ya Spartak Rotterdam na kuanzia hapo amekuwa akitafuta timu mpya ndipo KFC waliamua kumuita kwa ajili ya majaribio.

Baada ya majaribio ya wiki kadhaa, kocha wa klabu hiyo amesema kwamba nyota huyo ana kilo nyingi sana haswa kwenye mapaja yake na hivyo hawawezi kumsaini nyota huyo.

Mathias amekuwa akitemwa mara nyingi katika timu anazoenda kutokana na uwezo wake wa ufungaji na hadi sasa akiwa na miaka 28 tu amewahi kuzichezea timu 7 za wakubwa.

Haya ni kama majanga kwa familia yao kisoka kwani wakati yeye akikatiliwa, ndugu yao ambaye yuko United Paul Pogba naye kwa sasa hapikiki chungu kimoja na kocha wake Jose Mourinho.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here