Home Kimataifa VAR kufanyiwa majaribio EPL

VAR kufanyiwa majaribio EPL

9243
0

Huku na kule na huku na kule, vuuup VAR inahitajika England. Unakumbuka lile sakata wa kombe la dunia na VAR zao? Wengine wakasema inaboa, wengine wakasema haifai. Basi ndugu zangu niwataarifu kuwa Waingereza paaam nao wanaitaka.


Shirikisho la soka la FA inasemekana nao wanahitaji huduma ya VAR. Lakini waingereza wao bwana wameweka kipimo.  Wamesema watijaribu kwa mechi 15.

Wanadhani VAR itaondoa sakata la makocha kuwalalamikia marefa hasa baada ya Man City kufungwa bao la mkono na Wolveshampton.

Makocha kama Jose Mourinho wamekuwa wakilalamika kuwa vilabu vyao vimekuwa na bahati mbaya na maamuzi ya marefa.

 

Sio kwamba FA nao wanaikubali kiviiile,, hapana. Wanajaribu kuona je itatatua changamoto zao au ndio itawajazia nzi. Mimi nasubiria tu nione itakuwaje.

Natamani kusikia hata TFF nao wanaitaka

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here