Home Kimataifa Vardy na Cahil “Inatosha sasa”

Vardy na Cahil “Inatosha sasa”

8437
0

Jamie Vardy na Gary Cahill wamesema sasa inatosha kwa Three Lions


Jamie Vardy: the Fleetwood Town story

England imepoteza wachezaji wake muhimu wawili Jamie Vardy na Gary Cahill walioamua kuachana na soka la kimataifa.

Mshambuliaji huyo waLeicester City Vardy ambaye ameichezea timu ya taifa michezo 26 alimwambia kocha mkuu wa England bwana Gareth Southgate kuwa hatoendelea kubakia na kikosi hicho. Alimweleza hayo akiwa na timu ya taifa ya England katika kombe la dunia kule nchini Urusi.

“Suala hili limekuwa kwenye kichwa chnagu kwa kipindi kirefu” Alisema straika huyo mwenye miaka 31 alipokuwa kihojiwa najarida la the Guardian .

“Kiukweli kama unavyoona kuwa umri wangu unakwenda na mwalimu alikuwa akichagua zaidi vijana wadogo suala ambalo ni jema pia hasa kwa kombe la dunia”

Vardy, alipata fursa ya kuichezea England mchezo wake wakwanza dhidi ya  Republic of Ireland mnamo June 2015, mwaka huu aliichezea England michezo 4 katika michuano ya kombe la dunaia ambapo waliishia hatua ya nusus fainali. at this summer’s World Cup, where they reached the semi-finals.

Alimweleza mwalimu wa wake kuwa anahitajimuda mwingi na klabu yake pamoja na familia yake.

“Gareth alinieleza kuwa bado taifa linanhitaji akaniomba nibadilishe maamuzi lakini nimemuahidi kuwa nitakuwa tayari pale itakapotokea dharura,” alisema Vardy, ambaye amefunga mabao 7 akiwa na jezi ya timu ya taifa ya England.

Mashindano  M  G  A  Y YR   D
Jumla: 26 7 2 1 1.322′
12 5 1 731′
4 157′
4 1 83′
3 1 1 187′
3 1 164′

“Ikitokea dharura kubwa kama majeruhi na mwalimu akakosa mbadala siwezi kukataa kurudi kundini.”

Mlinzi wa Chelsea Cahill, mwenye miaka 32, ambaye amefunga mabao 5 kwenye michezo 61 akiwa na timu ya taifa nae pia ameamua kutundika daruga. Cahil alianza kuichezea England tokea mwaka 2010na amekuwa nahodha kwenye michezo kadhaa. Alicheza mchezo mmoja tu katika kombe la dunia kwenye kipigo cha 1-0 kutoka kwa Belgium.

“Nadhani huu ni muda muafaka kwa vijana wadogo kupata nafasi” alisema hayo akiongea na kituo cha Chelsea TV.

“Najivunia sana kuiwakilisha timu yangu ya taifa na kwa sasa napumzika kidogo ingawa sijaondoka moja kwa moja”

“Ikitokea shida yeyote nipo tayari ila kwa sasa acha vijana wapate nafasi kwanza mengine baadae.”


Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here